Kalonzo Musyoka, kinara wa WIPER//FACEBOOK

KINARA wa chama cha upinzani cha WIPER, Kalonzo Musyoka amefunguka kwa mara ya kwanza kuhusu maisha yake ya Kibinafsi, haswa ndoa yake.

Katika mahojiano ya kipekee nyumbani kwake na TV47, Musyoka alifichua jinsi alimkuta Pauline, mkewe miaka zaidi ya 40 nyuma kabla hata hajaingia kwenye siasa.

Alifichua kwamba walichumbiana na mke wake kwa miaka 13 na baada ya kuchaguliwa kama mbunge wa lililokuwa Eneobunge la Kituo Kaskazini, alichukua chini ya miezi 9 tu kumuoa rasmi.

“Nilichaguliwa kwenda bungeni 1985 baada ya kupoteza uchaguzi wa 1983. Eneobunge langu ya Kituo North wakati huo lilinichagua nikiwa kapera. Nilishinda uchaguzi Aprili na Desemba mwaka huo nilihakikisha nimeoa kwa sababu nilikuwa nimechumbiana na mke wangu kwa miaka 13,” Musyoka alifichua.

Mwanasiasa huyo wa muda mrefu alifichua kwamba mke wake kipindi hicho akiwa mpenzi wake alikuwa anampenda sana kiasi kwamba japo alikuwa anatoka katika Eneobunge tofauti, wakati wa kura alikuwa anahakikisha amepiga kura katika Eneobunge la Kalonzo ili kumpigia kura mpenzi wake.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Akizungumzia siri ya kudumisha muonekano wake wa ujana licha ya kuwa na umri wa miaka 71, Kalonzo alisema kwamba ni kujitunza vyema, huku akifichua kwamba hajawahi tumia sigara.

“Kwa kweli nimekuwa nikisisitiza kusema kwamba hufai kufanya kitu chochote kupita kiasi, sikuwahi kuwa mvuta sigara na mpaka leo hii sijawahi vuta sigara, sinywi pombe japo naonja-onja divai kidogo kwa sherehe za watu ili nisiwaangushe, lakini huwa sipendi,” alisema.

Alisisitizia watu kwamba jinsi unavyojiweka kimaisha huchangia pakubwa ukuaji wako kadri miaka inavyosonga.

Alisema kwamba muda wote amekuwa akisimama imara na sera yake ya kwamba mwanamume mkakamavu ni yule anayesimama peke yake.

“Wakati marafiki zangu wanalowa kwenye pombe na tuko kwenye hizo sherehe, mimi nilikuwa nalewa na soda, na hicho ndicho nimekuwa nikifanya tangu kitambo,” aliongeza.

Kalonzo, ambaye kwa sasa anasimama kama mwanasiasa mkuu wa upinzani humu nchini baada ya Odinga kuingia serikalini, amekuwa akijiweka tayari kwa kile anasisitiza kwamba 2027 huenda akawa debeni katika kinyang’anyiro cha urais.