
MSANII na mkurugenzi mkuu wa wakfu wa Simple Boy, Stevo Simple Boy amewaonya wanaume wanaotafuta wanawake wa kuoa dhidi ya kukimbilia wale wanaojitambulisha kama wameokoka.
Akizungumza na Obinna TV Updates, Stevo Simple Boy alisema kwamba siku hizi ni rahisi sana kupata mwanamke ambaye ni mtiifu, anamuogopa Mungu lakini bado akawa si mke mwema.
Kulingana naye, mrembo anaweza akawa mke mwema bila hata ya kuwa mtiifu au mwenye ameokoka.
“Wacha niwaambie kitu kimoja, unaweza pata msichana ameokoka, ni mtiifu, lakini bado asiwe mke mwema,” Simple Boy alisema.
Msanii huyo mwenye misemo na Kauli za kutatanisha alionekana kuegemea dhana kwamba kuna uwezekano wa kupata mwanamke anayetumia dawa za kulevya lakini akaibukia kuwa mke mwema.
Msanii huyo hata hivyo alisema ukifika wakati wake wa kutafuta mke, ataangalia vigezo vya utiifu, unyenyekevu na mchapa kazi.
“Mimi kwa sasa sitafuti mtu lakini ukifika huo wakati, kwanza lazima awe mchapa kazi, mchamungu, na mnyenyekevu,” alisema.
Akijibu kwa nini amekawia kupata mchumba, msanii huyo alisema kwamba amekuwa na ugumu kumpata ambaye atampenda yeye kama Stephen wa maisha halisi na si Stevo wa mitandaoni.
“Mimi siwezi sema eti naona sai wala mtondogoo, yule mwenye atakuja si eti anakuja juu ya Stevo Simple Boy, akuje juu anapenda Steven. Unajua Stevo Simple Boy ni wa mitandaoni na Stephen ni wa nyumbani,” alibainisha huku akikataa kabisa kuzungumzia uvumi wa kesi yake na aliyekuwa mkewe kuhusu suala la mtoto.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!