Rain
Mvua inatarajiwa kuendelea katika sehemu kadhaa za nchi hili ni kulingana na utafiti uliofanywa na idara ya hali ya hewa na mabadiloko ya nchi.

Nyanda za Juu Magharibi mwa Rift valley, Bonde la Ziwa Victoria, (Siaya, Kisumu, Homabay, Migori, Kisii, Nyamira, Trans Nzoia, Baringo, Uasin Gishu, Elgeyo-Marakwet, Nandi, Nakuru, Narok, Keriko, Bomet, Kakamega, Vihiga, Bungoma, Busia na Magharibi Kaunti za Pokot zitapokea mvua chache nyakati za asubuhi.

Maeneo hayo pia yanatarajia mvua kumwa wakati wa jioni ikiandamana na ngurumo za radhi kwa siku tano mfululizo kuanzia leo Alihamisi hadi jumatatu ijayo. Baadhi ya sehemu za kaunti hizo zitapokwea asilimia chache ya mvua mwendo wa usiku.

Kaskazini-magharibi (Turkana na Kaunti ya Samburu}, Maeneo haya yatapokea miale ya jua kwa asilimia kubwa. Mvua ikitarajiwa kunyesha kwa asilimia chache sana nyakati za jioni.

Nyanda za juu mashariki mwa Bonde la Rift [pamoja na Kaunti ya Nairobi, Nyandarua, Laikipia, Nyeri, Kirinyaga, Murang'a, Kiambu, Meru, Embu na Tharaka, zitapokea mvua chache kwa baadhi ya maeneo. Nyakati za asubuhi kutakuwa na mawingu mazito yatakayoziba miale ya jua katika baadhi ya maeneo.

 Kaskazini-Mashariki (Marsabit, Mandera, Wajir, Garissa na kaunti ya Isiolo zitapokea mvua kwa asilimia ndogo kuanzile leo, kesho na kesho kutwa. Kutakua na joto kati ya nyuzi 16 - 38.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Taita Taveta kaunti vile vile Sehemu  Mto wa Tana pia zitapokea mvua kwa asilimia ndogo katika baadhi ya sehemu hizo.

Pwani (Mombasa, Kilifi, Lamu na Kaunti za Kwale na pwani Sehemu za Kata ya Mto wa Tana.) Maeneo haya yatapokea mvua ya rasharasha nyakati za asubuhi, jioni , na usiku. Katashuhudiwa joto la kadri katika maeneo hayo kati ya nyuzi 24 - 35.