Gavana wa Nyeri Mutahi Kahiga alimkaribisha Rais katika ngome yake licha ya msimamo wake wa awali.

Katika ziara ambayo  ilingoa nanga hapo jana na Rais Ruto Katika eneo pana la Mlima Kenya na amabayo inakadiriwa kuchukua siku tano,kinyume na matarajio ya wengi kuwa ingemuwia vigumu kwa Rais Ruto kutwaa eneo hilo.

Safari yake iliyoanzia katika Gatuzi la Laikipia  Nanyuki kwa uzinduzii wa  miradi ya maendeleo mbalimbali pamoja na kutangamana na watu rais aliweza kupokelewa na wananchi wengi waliomkaribisha kwa shangwe vifijo na nderemo.

Hatimaye  Rais alifululiza moja kwa moja hadi ngome ya aliyekuwa naibu wake wa rais bwana Rigathi Gachagua Kaunti ya Nyeri kwa ajili ya uzinduzi wa miradi mbalimbali na utoaji wa vyeti vya mashamba.

Katika ngome hii ya Nyeri aliweza kukaribishwa kwa mikono miwili na Gavana Mutahi Kahiga ambaye ni mwandani na rafiki wa dhati sana wa bwana Rigathi  Gachagua ambapo kwa muda mrefu uliopita Mutahi amekuwa mwiba mkuu katika serikali ya Kenya Kwanza.

Itakumbukwa wazi kuwa mwaka jana kabla ya Rigathi Gachagua kutimuliwa alikuwa akidai kuwa serikali ya Kenya Kwanza ilikuwa ikimdunisha na kumudhalilisha kiongozi huyo kwa kutompa heshima zake jinsi anavyositahiki kupewa.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Hata katika hoja na mchakato mzima wa kumbandua mamlakani Rigathi Gachagua Gavana huyo alionekana kuwa mtetezi mkuu na kuweza kulaani mbinu zozote za aina hiyo za kutaka kumbandua mamlakani akiseema kuwa tukio au kujarbu mpango huo kungesababisha taifa kugawanyika kwa misingi ya Kikabila na hivyo kungetokea machafuko mabaya sana ya viita.

Lakini yote  tisa kumi ni kuwa baada  ya muda wa takribani miezi sita Rais aliazimia kuzuru ngome yake ya Mlima Kenya eneo lililompa wingi wa kura na kumhakikishia ushindi mnono katika uchaguzi uliopita wa mwaka wa 2022 na kutangazwa mshindi na kuwa amri jeshi mkuu wa majeshi yote ya ulinzi.

Kumbuka kabla siku ya jana na kwa muda wa miaka miwili iliyopita Serikali ya kENYA kwanza imepitia changamoto tele jambo ambalo liliweza kuishusha chini serikali ambayo ilikuwa ikizungumzia maisha ya mwananchi wa kawaida ilibadili ajenda na kutekeleza kanuni ambazo  ni dhalimu na ambazo ziliweza kuleta hali tete nchini raia wengi wakipinga sera hizo dhalimu kama kutozwa ushuru mwingi.

Mwaka wa 2024 mwezi wa juni kulizuka maandamano ya  vijana wa kizazi cha Genz-  Z waliopinga mswada wa fedha wa 2024/2025 na kuandamana hadi kuingia katika bunge la Taifa na kusababisha Rais kuufutilia mbali na hatimaye kuvunja baraza lake la mawaziri lote.

Hata hivyo yaliopita si ndwele Gavana Mutahi alimchangamkia Rais kwa kile alikitja kama siasa kando maendeleo mbele.

''Watu wa Nyeri mmefurahia kumkaribisha Rais nyumbani? Wapi makofi ya Rais ya kumkaribisha nyumbani'' bwana Mutahi alisema na wananchi waliomshangilia kwa kumkaribisha Rais  nyumbani akisema kuwa walichangia pakubwa kwa serikali hio kwa hivyo ilikuwa vyema kwao kumkaribisha Rais na kufurahia maendeleo kama wakenya Wengine.

Ni hatua nzuri kwa bwana Mutahi Kahiga kwa kuonyesha  siasa komavu tena yenye demokrasia kwa kushirikiana na Rais kwa manufaa ya Kuleta maendeleo mashinani.