Djed Spence, Tottenham Hotspurs Player with originality of Kenya, Jamaica ana England
Mshambuliaji wa zamani ya timu ya taifa ya Kenya Harambee Stars Taiwo Atieno amemuomba beki wa wa Tottenham inayoshiriki ligii ya uingereza kuwaza kuhusu kuwakilisha Kenya.

Amemtaka mchezaji huyo kuwakilisha Kenya hasa kwenye michuano ijayo ya kufuzu kwenye mapambano ya kombe la dunia  wakati ambapo nafasi yake ya kuiwakilisha uingereza kwenye timu ya taifa ni finyu baada ya kuachwa nje na mkufunzi Thomas Tuchel.

"Tofauti sana na uingereza, mahali ambapo kuna talanta nyingi hasa mabeki wa pembeni. Kenya itampa Djed Spence nafasi nzuri sio tu uwanjani bali pia katika mpira wa baadaye wa Kenya," alisema Atieno.

"Kenya inapoendelea kung'ang'ana kufuzu kombe la dunia kwa mara ya kwanza, Djed anaweza ongoza kizazi hiki na awache historia nizuri sana nchini Kenya na Afrika. Neno langu ni kwamba Djed awazie zaidi kuhusu kuwakilisha Kenya sababu ana nafasi nzuri ya kuandika historia ambayo haijawahi kuwepo. Kitu ambacho kitakuwa kigumu sana kufanya akiwa Uingereza,"  alieleza zaidi.

Spence, ambaye ana haki ya kuchezea England, Kenya na Jamaica, anakabiliwa na kufanya maamuzi magumu ya kuchagua timu ya taifa ya kuwakilisha.

Beki huyo, ambaye kwa sasa yuko katika hali nzuri na anaonesha mchezo mzuri alikosa nafasi kwenye kikosi cha Tuchel cha kuiwakilisha Uingereza.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Baada ya kukosekana kwa Spence kwenye vikosi vya zamani vya England hapo awali kuliibua maswali juu ya ikiwa anaweza kubadili mawazo na kujiunga na  Harambee Stars ya Kenya, ambapo angeweza kupata nafasi ya kuanza moja kwa moja kutokana na kiwango chake cha juu cha kucheza soka ila aliwahi kunukuliwa akisisitiza kwamba lengo lake ni kuiwakilisha uingereza siku zijazo.

"Ni nani asiyependa kucheza kwa ajili ya nchi yake? Hiki ni kitu ambacho ninakisubiri kwa hamu. Ikiwa nitaitwa, itakuwa furaha, kama sitafanikisha, nitaendelea kufanya kazi kwa bidii," aliwaambia wanahabari.

Pamoja na mafanikio yake ya kuvutia kwa Tottenham, mlinzi huyo bado ana matumaini kwamba kazi yake nzuri itatambuliwa katika ngazi ya kimataifa ila haifahamiki iwapo atabadili mawazo ya kuondoka uingereza na kuchagua upya kati ya Kenya na Jamaika.

Kwa sasa, mtazamo wa Spence unabaki kwenye soka la klabu, lakini kujitolea kwake kwa England kunaashiria mwelekeo wazi kwa kazi yake ya kimataifa siku za baadaye.