Gavana wa Kakamega mheshimiwa Fernandes Barasa alizindua mpango wake maalum wa kugawa na kusamabaza mbolea katika kaunti Nzima.
Katika chapisho rasmi kwenye ukurasa wake wa X bwana Barasa aliazimia kuwagawia wakulima mbolea pamoja na mbegu za upanzi huku mpango huo ukilenga wakulima walio na mapato ya chini na familia sizizojiweza.
Mbolea hio pamoja na mbegu za upanzi zinawa kugawiwa kwa wajane na watu walio na upungufu wa viungo vya mwili(walemavu) ili wafaidi kutoka kwa usimamizi wa Kaunti.
Huo mpango unalenga kusambazwa katika maeneo yote ya maeneobunge 12 eneo bunge la Matungu likiwa ni la kuanza kupokea mbolea hiyo ya Kaunti , mpango huo umeanzia katika eneobunge la Matungu ambapo wajane ,watu walemavu na familia sisizojiweza zimepewa kipaumbele kuweza kunufaika pakubwa katika mradi huo wa mbolea ya bei nafuu.
Gatuzi la kakamega lina maeneobunge kumi na mawili 12, Matungu,Mumias magharibi,Mumias Mashariki,Butere, Khwisero, Shinyalu,Lurambi,Ikolomani,Likuyani,Lugari,Malava na Navakholo.
Mpango huo unajiri wakati ambpo wakulima wako mbioni kuhakikisha kuwa wanapata mboea ili kuanza shughuli ya upanzi ambapo msimu wa unpanzi tayari umekwisha ngoa nanga.
Hata hivyo bodi ya nafaka na mazao nchini NCPB ilikuwa imewatangazia wakulima kuwa tayari mbolea ilikuwa kwenye maghala yake kwa hivyo wakulma walikuwa huru kuenda kununua mbolea huku wakiwa wanajiandaa ni kwa ajili ya upanzi.
Hata hivyo katika bodi ya nafaka na mbolea kumeripotiwa visa vya baadhi ya madalali ambao wameripotiwa kuwa katika mstari wa mbele kununua mbolea hiyo na kuificha ili kuwapunja wakulima kwa bei ya gharama ya juu wakati ambapo mbolea hiyo itahitajika wakati wa upanzi.
Katika sehemu za Kitale Kaunti ya Trans Nzoa Kuliripotiwa visa vya matapeli kuchulia fursa ya kuepo kwa mbolea na badala yake kupakia mbolea ambayo ni mchanga jambo ambalo umma ulilalamikia na kuirai serikali kuwa macho ili kuweza kuwakamata walaghai hao.
Kilimo cha mahindi kwa historia pana kimekuwa ndicho nguzo muhimu sana katika maeneo ya magharibi ya Kenya huku wakulima wengi wakishiriki pakubwa katika kilimo hicho hivyo kuongeza kiwango cha mazao nchini ambapo kilimo ndicho uti wa mgongo wataifa.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!