Gloria Orwaba

Seneta maalum Gloria Orwoba ameeleza juhudi zake za kupigana na changamoto zinazokuja kwake hasa kutoka kwa maisha ya kawaida.

Seneta huyo anayewakilisha wanawake bungeni amefichua kwamba wakati mwingine mambo ya uongo yanaweza kukukatia  tiketi na kukupandisha ndege ila ukweli ni tofauti kabisa.

"Uongo utanunua tikiti, kupanda ndege na kuruka maelfu ya maili kabla ya ukweli kuzima alama ya kengele inapokuamsha," Alisema Orwoba.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

"Katika maisha ya ukweli, kila kitu kimewekwa ili kukupunguza au hata kukufunga. Media itauza simulizi yako ambayo hata hukujua ipo. Watahakikisha wamechagua na kuhariri picha zako mbaya zaidi ili uweze kuonekana kama mtu mbaya zaidi," alieleza.

Mwanasiasa huyo amewataka watu kutotishika na changamoto zinazokuja badala yake kujiamini kwamba wanaweza. Ameeleza kwamba hakuna mtu mwingine ambaye anaweza kuwepo kwa ajili yao maana maisha ni mtu mwenywewe kujitengenezea.

"Lakini hapa lazima ukumbuke kila wakati; wewe ndiye mtu bora zaidi anayeweza kuwa katika bustani hiyo yako ndiyo sababu huwezi kutosheka kujihusu. Kuna kitu unachofanya kila wakati ambacho hufanya jitihada iendelee kwa hivyo usigome," alitoa kauli seneta huyo.

Wakati huo huo pia ameendelea na kuandika kwenye mtandao wake akiwahimiza watu wanaotaka kufika mbali kutokuwa wepesi wa kukata tamaa wakati changamoto zinapokitiri.

"Haijalishi wanasema nini, fanya au kuandika nini juu yako, endelea. Kuna idadi kubwa ya watu ambao wako kimya na wanakukusudia  kufanikiwa katika juhudi zako. Weka umakini, na ujikaze zaidi wakati unataka kuacha... sio wakati wanataka uache," alisistiza.

Mwanasiasa huyo aliwahi kujipata katika changamoto kadhaa za maisha ikiwemo kufukuza kwenye bunge la seneti na kukaa inje ya vikao kwa zaidi ya miezi mitatu.