Kalonzo Musyoka

Kinara wa Wiper Kalonzo Musyoka ameelezea msimamo wake kuhusu mchakato mzima unaoendelea wa kumtafuta mwenyekiti wa IEBC pamoja na makamishina..

Kinara huyo wa Wiper alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari alijibu maswali kutoka kwa wanahabari kwa kusema kuwa wao kama upande wa upinzani mchakato uteuzi wa makamishina wa IEB C  unawahusu pakubwa sana.

Musyoka kulingana na mujibu wa maelezo yake alidokeza kuwa alikuwa amewaandikia barua  kinara wa chama cha ODM bwana Raila Odinga halikadhalika na Rais William Ruto akiwaelezea jinsi suala hilo la uteuzi ni la muhimu sana na lilikuwa likihitaji kila mtu kupewa nafasi ya kujieleza pale anapohisi hapaendi vizuri.

Kalonzo alisema kuwa wao kama washikadau katika suala  kuu la uchaguzi wana ari na umuhimu sana pia kufuatilia na kutaka kujuwa kila kitu ambacho kilikuwa kikijiri bila kunyamaza.

''Sisi kama viongozi wa upinzani hatutasalia kimya wala kukaa kitako tukingoja tume ambayo inawahoji makamishina ikichukua mkondo mbaya wala kuanza kutoa maamuzi ambayo yanaegemea upande mmoja wa Rais Ruto na tumekimya hatuwezi''. Kalonzo alisema.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

''Mnavyojua ni kuwa wakenya wangali wana machungu na hasira kuu kutokana na uchaguzi wa mwaka wa 2022 ulivyoendeshwa bila uwazi na ukafanya wakenya wengi kupandwa na mori hadi leo kwa hivyo zoezi hili ni la muhimu sisi sote'' Kalonzo alieleaza.

Wakati ambapo Kalonzo anaendelea kutoa usemi wake wanajopo wa  kuwakagua makamishina wa IEBC bado unaendelea kwa Juma la pili sasa  huku zoezi hilo likitarajiwa kukamilika mwezi ujao.

Itakumbukwa wazi kuwa awamu ya kuwahoji waliokuwa wakiwania nafasi ya mwenyekiti ilikisha kamilika sasa itakuwa ni awamu ya kuwapiga msasa makamishina wa tume hiyo ya IEBC ili kupata jumla ya makamishina tiisa ambapo majina yao yatapendekezwa kwa rais ili afanye uamauzi wa mwisho.

Shughuli nyingi za masaula ya uchaguzi zilisimama kutokana na kukosekana kwa tume ya uchaguzi ambayo inastahlili sasa kuwa ilikishaundwa ili kuhakuiikisaha deta za wapigakura zinakagulia uipasavyo na kuhakikis,hakuwa inaanza kuangazia wapiga kura wengine wapya.

Hata hivyo kuna sehemu mbalimbali ambazo zinahitaji kufanyiwa uchaguzi mdogo kutokana na kuaga dunia kwa viongozi shikilizi au kutokana na kuteuliwa katika nyadhifa mbalimbali mfano ni eneobunge la Ugunja, Malava na Mbeere Kasikazini ambapo hakuna viongozi wanaostahili kuwawakilisha.