caption
Mshambuliaji wa Manchester City Erling Haaland anakabiliwa na kipindi cha matatizo kutokana na jeraha la kifundo cha mguu [ankle injury] klabu hiyo imethibitisha.

Mshambuliaji huyo alilazimishwa kuondoka katika kipindi cha pili cha ushindi wao wa Kombe la FA huko Bournemouth, ambao City ilishinda 2-1.

Haaland baada ya kuumia na kuondolewa uwanjani nafasi yake ilichukuliwa na Omar Marmoush, ambaye alifunga bao lililowapa  ushindi ndani ya dakika chache baada ya kuwasili kwake.

Haaland aliondoka kwenye Uwanja akiwa amevalia buti ya kinga na magongo kama tahadhari. Alifanyiwa vipimo jana Jumatatu na klabu hiyo imethibitisha kuwa amepata jeraha ambalo litamwondoa uwanjani kwa muda.

Hatacheza dhidi ya Leicester City Jumatano na bila shaka sasa atakosa Manchester derby wikendi hii. City wanatarajia kuwa atakuwa salama kabla ya kumalizika kwa kampeni za msimu huu, lakini muda bado haujulikani hadi mchezaji huyo afanyiwe vipimo zaidi.

Taarifa ya klabu ya Mancester City illisema: "Manchester City FC imeweza kuthibitisha kuwa Erling Haaland amepata jeraha kwenye  mguu wake wa kushoto.

Mshambuliaji huyo wa Norway alipata jeraha hilo wakati wa ushindi wa robo fainali wa Kombe la FA Jumapili ugenini dhidi ya AFC Bournemouth. Erling alifanyiwa vipimo vya awali huko Manchester Jumatatu asubuhi na sasa atatafuta ushauri wa kitaalam ili kuthibitisha kiwango kamili cha jeraha hilo

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Tathmini bado inaendelea ili kubaini ubashiri kamili. Matarajio ni kwamba Erling atakuwa sawa ili kucheza sehemu zaidi katika kipindi kilichosalia cha msimu huu, ikiwa ni pamoja na Kombe la Dunia la Klabu la FIFA msimu huu wa joto.

Erling Haaland amefunga mabao 21 katika mechi 28 hadi sasa katika msimu wa Ligi Kuu ya 2024/2025. Mabao 11 kati ya 21 yalifungwa nyumbani huku akifunga mabao 10 kwenye michezo ya ugenini. Kwa ujumla, mabao ya Erling Haaland yaliyofungwa kwa dakika 90.