KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumapili, Machi 30, 2025..

Katika taarifa ya siku ya Jumamosi jioni, kampuni hiyo ilitangaza kwamba baadhi ya maeneo ya kaunti mbili za Kenya yatakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Kaunti ambazo zitaathirika na kukatizwa kwa umeme ni Nairobi, na Uasin Gishu.

Katika kaunti ya Nairobi, sehemu za maeneo ya Gikomba, Kamukunji, na Eastleigh zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Sehemu za maeneo ya Soy, Chemoset, Kabobo, Nangili, Kongoni, CMC Motors, na Pan Villa katika kaunti ya Uasin Gishu pia zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.