KIPCHUMBA MURKOMEN
Waziri wa usalama wa ndani Kipchumba Murkomen ametangaza kuwa Jumatatu, Machi 31, 2025, itakuwa siku kuu ya kitaifa.

Murkomen ametangaza hili kupitia tangazo kwenye gazeti rasmi la serikali siku ya Ijumaa, Machi 28,  ili kuwapa Waislamu muda kuadhimisha siku kuu ya Idd-ul-Fitr.

"Imeafikiwa kwamba, katika kutekeleza mamlaka yaliyotolewa na kifungu cha 2 (1) cha Sheria ya likizo za umma, waziri wa usalama na mambo ya ndani na Utawala wa Kitaifa natangaza kwamba Jumatatu, tarehe 31 Machi, 2025, itakuwa likizo ya umma kuadhimisha Idd-ulFitr," ilani hiyo ilisema.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Idd-ul-Fitr ni sikukuu ya kwanza kati ya mbili rasmi zinazoadhimishwa na dini ya kiislamu.

Idd-ul-Fitr inaadhimishwa na Waislamu duniani kote kwa sababu inaashiria mwisho wa mfungo wa mwezi mzima wa alfajiri hadi machweo ya Ramadhani. Inaadhimishwa wakati wa siku tatu za kwanza za Shawwāl, mwezi wa 10 wa Uislamu.

Idd al-Fitr ni wakati wa mapokezi rasmi na ziara za kibinafsi, wakati marafiki wanasalimiana, zawadi hutolewa, nguo mpya huvaliwa, na makaburi ya jamaa yanatembelewa.

Kufuatia tamko la Murkomen, ofisi zote za serikali, shule, na taasisi zingine kama benki zinatarajiwa kufungwa kuadhimisha sherehe hiyo ya kidini.

Ramadhani ilianza jioni ya Ijumaa, Februari 28, 2025 na inatarajiwa kuhitimishwa jioni ya Jumamosi, Machi 29.