Francis Atwoli, aktibu mkuu wa COTU//X

KATIBU mkuu wa muungano wa wafanyikazi COTU, Francis Atwoli amefichua kwamba likizo ya uzazi kwa wafanyikazi wa kiume humu nchini ni moja ya kazi yake.

Atwoli, kupitia ukurasa wake wa X alifichua haya alipokuwa akimjibu aliyekuwa gavana wa Makueni profesa Kivutha Kibwana ambaye alikuwa ametaka COTU kumpa katibu wao likizo ya ubaba.

Kibwana alianza kwa kumhongera Atwoli kwa kuwa baba mpya mjini, shukrani kwa mkewe Mary Kilobi aliyejifungua mtoto wa kiume – Atwoli Junior.

“Ninaipongeza kwa moyo wote familia ya @AtwoliDza kwa ujio mpya katika familia yao. @COTU_K wanapaswa kumpa Katibu Mkuu wao Likizo ya Ubaba inayostahiki ambapo wanaweza pia kujadili: Je, COTU na uongozi wa vyama vya wafanyakazi unapaswa kuwa suala la umiliki wa maisha?” Kibwana alihoji.

Akimjibu, Atwoli alianza kwa kufafanua kwamba amepigania wafanyikazi wa kiume kupata likizo ya ubaba ambayo miaka ya nyuma haikuwepo.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Atwoli alidokeza kwamba ni kutokana na juhudi zake ambapo likizo ya ubaba ilisimikwa rasmi kwenye katiba ya Kenya ya mwaka 2010.

“Kwanza, nimepigania wafanyikazi [wa kiume] wa Kenya kupokea likizo ya uzazi kama sehemu ya kazi yangu kuleta seti tano (5) za sheria za Kazi. Unatambua kwamba sheria hizi na Katiba ya Kenya 2010, kama ilivyo katika Kifungu cha 41, zimempa mfanyakazi Mkenya mamlaka zaidi ya yote katika eneo hili,” alisema.

×

Kuhusu swali la Kibwana kutaka kujua kama ukatibu wa COTU ni kazi ya kudumu ya Atwoli, katibu huyo ambaye ameshikilia uongozi wa COTU kwa takribani miaka 24 alimwambia kwamba hata yeye amemuona Kibwana akipewa kazi ya kufunza chuo kikuu licha ya kuwa mwanarika wake na kutaka kujua kama yake pia ni ya kudumu.

“Pili, mimi na wewe ni marafiki wa umri. Na nilikuona tu ukiteuliwa kuwa profesa wa Sheria katika Chuo Kikuu cha Daystar hapo juzi. Hivi Prof, nieleweshe, taaluma yako inaisha lini? Hivi kweli profesa anaweza kuacha kusoma, kufundisha na kuandika? Utaacha lini kushirikisha akili yako?” alimjibu kwa njia ya swali.

Mapema wiki hii, Francis Atwoli,75, aliripotiwa kukaribisha mtoto na mkewe Mary Kilobi, 40, baada ya kuwa katika ndoa kwa takribani miaka 7.