
MBUNGE wa Mumias Mashariki Peter Salasya ameendelea kupoeromosha machungu yake kufuatia kushambuliwa wikendi iliyopita ugani Nyayo wakati wa mechi kati ya Kenya na Gabon.
Mbunge huyo ameendeleza mashambulizi ya maneno kwa wale waliomshambulia, ambao sasa amewataja kuwa wazee kumliko ambayo hawana aibu.
Kwa mujibu wa Salasya, ni aibu sana kuona watu waliomshambulia wengi wao wanamzidi kiumri, akijitetea kuwa yeye ni mtoto mdogo kwao.
Salasya alisema kwamba yeye ni kijana Gen Z ambaye mara nyingi huongea kuwakilisha kizazi hicho na kuona ‘wazee’ wa miaka 40 na zaidi wakimshambulia ji jambo la aibu.
“Ukiangalia watu ambao walishambulia Peter Salasya, ni watu ambao wengi wao wako katima umri wa miaka 40s, sasa ukiangalia wao si Gen Z na ni watu ambao hawana itikadi za Gen Z na wanapiga mtoto mdogo mimi si ni aibu,” Salasya alisema.
Mbunge huyo pia alimkosoa vikali mkereketwa wa siasa za Raila Odinga, Gaucho akimtaja kama mtu mkubwa hata kumliko na ambaye hafai kuzungumza kwa niaba ya vijana.
“Wananishinda na wanakuja kupiga mtoto mdogo kama mimi ambaye amejituma. Nataka kuwaambia wale jamaa huu mwili wangu umepigwa sana mpaka kufika penye nimefika,” aliongeza.
Salasya alirejelea Kauli yake ya awali kwamba katika vipigo amekuwa akipokezwa kutoka siku za nyuma, kila ambaye alishiriki katika kumpiga hakubaki salama.
“Kila mtu ambaye alinipiga alikufa, kama unagusa mwili wangu unakufa. Hiyo ndio maana siwezi mshtaki yeyote. Na kusema ukweli, tangu nianze kupokea vichapo sijawahi mshtaki mtu. Huwa naacha hukumu asili kuchukua mkondo wake, lakini pia ninawaonya kwamba wasizoee [kunipiga piga]. Wakati mwingine utafikiria eti Peter Salasya hawezi kuthuru na ukuje upate pengine maneno yameharibika,” alimaliza kwa onyo.
Mbunge huyo alishambuliwa pindi tu baada ya kufika uwanjani, na baadae alionekana kulaumu mashambulizi hayo kwa misimamo yake mikali dhidi ya siasa za Raila Odinga.
Salasya amekuwa akikosoa vikali Odinga, haswa baada ya kufanya ubia na rais Ruto ambapo ODM na UDA vilitia saini mkataba wa kushirikiana pamoja hadi 2027.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!