Kiranja wa walio wengi  katika bunge la taifa Silivanus Osoro alisema kuwa alipoteza wazazi wake katika umri wa miaka saba.

Alikuwa akisimulia hali hio akimfariji Mbunge wa Dagoretti Kasikazini kutokana na  msiba wa kumpoteza mtoto wake katika ajali ya barabarani.Marehemu Elivis aliaga kwa  kuhusika katika ajali ya barabarani akiwa katika safari yake kuelekea upande wa kasarani.

Osoro aliweza kusimulia kwa kusema kuwa baada ya kuwapoteza wazazi wake alisalia yatima asiye na wa kukimbilia wala kulilia lakini baadaye aliweza kupokea tena upendo wa mama baada ya Beatrice Elachi kumchukua.

''Wakati ambapo nilipoteza wazazi wangu nikiwa na umri wa miaka saba nilisalia kuwa yatima  ambaye hakukuwa na mbele wala nyuma nilikosa mtu wa kunifariji na kunionyesha upendo wa mama nikawa nimesononeka sana na kuwa na mawazo mengi'' Osoro alisema.

''Lakini kutokana na kuwepo kwa Beatrice Elachi aliweza kunipokea na kunipa  upendo wa mama, alinilea na kunionyesha upendo mkubwa sana ninamheshimu kwa kiwango kikubwa sana'' Osoro alisema.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Hata hivyo aliweza kusema kuwa baada ya kuchukulia maisha kuwa jambo la kawaida aliweza kusoma kwa bidii na kufaulu katika masomo yake na  hivyo kumpa nafasi ya kuchaguliwa kuwa kiongozi.

Katika bunge la  taifa  Osoro  alieleza kuwa hata awapo katika mabishamo ya kutetea na kupinga misuada mbalimbali hakuna siku amewahi mkaripia wala kubishabna na bi Elachi kisa na maana ni  heshima  komavu ya malezi ambayo anamiliki kutoka kwake.

'' Hata wakati mnionapo bungeni nikiwa nimewaka moto na kuonekana kama ninafarakana na  wabunge wenzangu hamna siku nishawahi mkaripia bi Elachi wakati ambapo tuko bungeni na hata  asimamapo kuweza  kupinga hoja  zangu mimi hutulia na kujifanya sijasema chochote  kuashiria heshima yangu na yeye.

Ajali hio ilitokea kutokana na gurudumu la gari kupasuka hivyo duru za kuaminika zilisema kuwa marehemu huenda alikanyaga breki ya ghafla jambo ambalo linakisiwa kuwa lilisababisha  gari kubingirika na kujigonga  katika ukuta wa uzio ulio kando ya barabara.

Hata hivyo marehemu alipopelekwa hospitalini aliweza kulazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi ambapo aliweza kuripotwa kuwa ameaga baada ya siku kadhaa, Marehemu aliaga akiwa na umri wa miaka 26 ambapo alikuwa mfano bora kwa vijana wa kiwango cha umri wake.