Aliyekuwa Jaji mkuu David Maraga alikubali wito wa vijana wa kizazi  cha  Gen Z kwa  kuitikia wito wa kumtaka kuwania  urais mwaka wa 2027.

Alizungumza akiwa katika  Kaunti ya Migori Katika chuo kikuu cha Rongo baada ya kuwahutubia wanafunzi kuhusu maswala mabalimbali yanayofungamana na uongozi. 

Jaji huyo wa Zamani aliweza kuelezea ari yake kuwa angependa tena  kuongoza mhimili mwingine wa serikali kama alivyoongoza mahakamani kama jaja mkuu kwa miaka minne na miezi mitatu tangu mwaka wa 2016-2021.

''Nimehudumu  mwanzoni kama Jaji mkuu katika jamuhuri ya Kenya kwa  hivyo sioni kama kuna ubaya  wowote mimi kuongoza mhimili mwingine wa serikali  kwa kuwa ni jambo zuri tena lenye tija katika  taifa  na kwa wananchi" Maraga alisema.

Kulingana na mujibu wa  maelezo yake Bwana Maraga  alionyesha  kuwa na  uzoevu katika masuala ya uongozi hivyo alikuwa na imani fika iwapo angepewa fursa ya kuliongoza taifa  bila shaka  angetekeleza wajibu huo  kwa kujitolea na kwa kuzingatia mwongozo wa katiba.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Hata hivyo aliweza kukosoa serikali iliyoko mamalakani kwa kuweza  kuunda  bajeti ya  taifa ambayo ni fisadi na  ambayo haioani na malengo wala mahitaji ambayo Wakenya  wanatilia kipaumbele.

Alisuta wale ambao huunda na kukadiria bajeti ya  taifa kwa kutotengea masuala muhimu pesa na kuangazia  masuala ambayo mwananchi  mlipa ushuru anakabiliwa nayo na  badala yake bajeti huundwa kwa  kuelekezea pesa nyingi kwa vitu ambavyo si vya muhimu sana  kwa mawananchi mlipa ushuru.

''Kwa sasa ninafanya ushirikiano na washikadau mbalimbali ili kuweza kufanya  tangazo rasmi kwa wananchi kuhusu msimamamo ambao nitakuwa nimeamua  lakini kile ambacho ninashutumu kwa kusema kuwa ni tatizo kubwa nchini  ni usfisadi  na kukuwa na  taasisi nchini ambazo ni fisadi''. Maraga .alisema.

Hata katika usanjari huo aliweza kuwarai wakenya kuishi kwa amani  na kuwa  katika mstari wa mbele kuwajibikia  vitendo  vyao na  vilevile kuonyesha mifano  miema katiaka uongozi  wao.

David si wa  kwanza kutoka jimbo la Kisii ambaye  ameonyesha ari ya  kuwania kiti cha urais nchini aliyekuwa waziri wa usalama wa ndani Daktari Fred Matingi na Mwanaharakati Morara Kebaso ni miongoni mwa  viongozi  ambao wameonyesha ari ya kuwania kiti cha Urais mwaka wa 2027 hata hivyo bwana Maraga anakumbuwa na wengi kwa kuwa jaji wa kwanza kufutilia mbali matokeo ya urais ya mwaka wa 2017.