Lillian Nganga//X

ALIYEKUWA mama wa kaunti ya Machakos Lillian Nganga ametilia shaka viwango vya elimu humu nchini, akihoji ni vipi Kenya ilijipata katika nafasi ya kuwa na watu wengi wenye uwezo wa kuandikwa na kusoma lakini hawajui kujieleza vizuri.

Kupitia ukurasa wake wa X, bi Nganga alidai kwamba vijana wengi nchini ni wasomi lakini wachache ndio wanajua kuandikwa na kujieleza vizuri.

“Inakuwaje kiwango cha watu wa Kenya kujua kusoma ni kikubwa, ilhali vijana wengi hawawezi kuandika na kujieleza vizuri?”

×

Mama huyo wa mtoto mmoja wa kiume aliyepata na rapa Juliani alisema kwamba tatizo hilo aghalabu lilianza baada ya kizazi cha Millenials.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Kulingana na Nganga, inashangaza sana kuona mabadiliko hayo makubwa ya kwamba watu wengi ni wasomi wasioweza kujieleza licha ya kutokuwa na mabadiliko makubwa ya utoaji wa elimu kati ya kizazi cha Millenials na Gen Z.

“Nadhani kupungua kulianza baada yetu (milenia), kwa hivyo nashangaa ni nini kilibadilika kwani msingi wa mfumo wa elimu haujabadilika kiasi hicho!” alihoji.

Nganga katika siku za hivi karibuni ameonekana kuzamia zaidi masuala ya siasa, akitoa maoni yake kuhusu siasa za Kenya bila kubabaishwa na mashambulizi kutoka kwa baadhi ya watumizi wa mitandao ya kijamii.

Wiki chache zilizopita baada ya kuweka wazi kwa mara ya kwanza kwamba penzi lake na Juliani lilikuwa limegonga mwamba, na akaweka wazi kuwa katika maisha yake tangu atomize miaka 25 hadi sasa anapokaribia kufikisha miaka 40, amekuwa na wanaume 2 tu.

“Je, ukweli kwamba nimekuwa na wanaume wawili tu tangu nikiwa na umri wa miaka 25 (ninatimiza miaka 40 mwaka huu) unawezaje kunifanya mambo yote ya kipuuzi mnayoniita? ? Pumbavu, Wajinga sana!” Lillian Nganga alichapisha.

Akirejelea uhusiano wa zaidi ya miaka 10 na aliyekuwa gavana wa Machakos ambaye sasa ni Waziri wa leba Alfred Mutua ambao ulivunjika mwaka 2021, Nganga alisema kwamba anajionea Fahari kuwa miongoni mwa watu waliosimama na mwanasiasa huyo katika kampeni mara mbili na kushinda ugavana naye.

Nganga aliyeonekana kusimama kidete pasi na kutetereka dhidi ya mashambulizi kutoka kwa wanamitandao alisema kwamba huo ni mwanzo tu na yeyote ambaye atashindwa kustahimili majibu yake basi ajiondoe mapema kwenye gumzo.