Georgina Njenga

MREMBO Georgina Njenga amekanusha madai ya kurejelewa kama malkia wa kivumbi kwenye mapenzi.

Japo hakukanusha bayana jina hilo la msimbo, Njenga alisema kwamba yeye hujawahi onesha mtu kivumbi katika mapenzi, akisema katika maisha yake ameingia katika huba mara mbili pekee.

Alisema kuwa pengine kuitwa malkia wa kivumbi katika mapenzi ni jina la msimbo ambalo anaweza kulilaumu kwa pombe.

“Eeei jameni, wacha tu niilaumu kwa pombe kwa sababu sijui nitafanya nini ingine? Penzi langu ambao watu wanajua lilivunjika ni moja tu – na Tyler Mbaya. Katika maisha yangu yote hata nimependa mara 2 tu,” alisema.

Hata hivyo, Georgina Njenga alisema kwamba kwa kiasi Fulani yeye ni ‘queen of dust’ kwani amekuwa akifukuzia mapenzi lakini mapenzi yanamuonyesha kivumbi, huku akikanusha kuwa ni yeye huwaonyesha vumbi wanaomfukuzia kwa mapenzi.

“Kwa kiasi Fulani naweza kuwa malkia wa kivumbi kwa sababu mimi ni mrembo wa mapenzi. Huwa natafuta mapenzi lakini mapenzi hayanitaki. Ushawahi ona ile unafika mpaka unajiambia labda mapenzi hayakuumbwa kwa ajili yako,” alijieleza.

Alipobanwa zaidi, mama huyo wa mtoto mmoja alinywea na kukiri japo kwa shingo upande kwamba yeye ni ‘queen of dust’ kwa kurejelea vitu ambavyo amepitia katika safari yake ya mapenzi.

“Watu wanapelekwa hadi Malaysia lakini wewe 50/50 na kule kuna mtu analipiwa kila kitu. Mpaka nashangaa Mungu mimi nilikosea wapi. Mimi nimeweka mtu si mara moja, basi mimi ni ‘queen of dust’. Mimi mpaka nimewahi tumia mwanamume pesa, jamani mniombee. Mmoja ilikuwa pesa ya maana lakini mwingine ilikuwa pesa ya kuchezea, na si eti pesa hivi hivi juu ako katika ndoa,” Georgina alidokeza zaidi.

Akirejelea Kauli yake kuhusu uhusiano na mwanamume aliyeko katika ndoa, Georgina Njenga alisema kuwa hakujielewa katika penzi lake kiasi kwamba alikuwa anamtumia pesa tu bila kujali.

“Ndio maana nawaambia mniombee, alikuwa ananiambia tu ‘niwekee mafuta’ na mimi mjinga namwekea. Na ako na gari wakati mimi sina lakini mafuta namwekea mimi. Na ako na mke wake na watoto wake. Sijui kama nilikuwa nimezama kwenye penzi lake,” Njenga aliongeza.