Naibu wa Rais Profesa Kithure Kindiki alisema kuwa serikali kwa sasa ina hela za kukamilisha miradi yote ya serikali iliyosimama tangu mwaka wa 2018 hadi 2019.
Alizungumza hayo alipokuwa katika Kaunti ya Tharaka Nithi eneo la Mucatha mnamo Alihamisi Machi 27, 2025. Katika mazungumzo yake aliweza kusema kuwa barabara husaidia sana kusafirisha bidhaa hadi kwenye masoko mbalimbali.
Barabara zinapokuwa sawa huweza kusababisha maisha ya Wananchi kuwa bora na mufti kabisa hivyo kuendeleza uchumi wa taifa.
'' Serikali kwa sasa ina malighafi ya kutosha ya kuweza kufufua na kukamilisha miradi yote ya serikali ambayo ilikuwa imekwama tangu mwaka wa 2018 hadi mwaka wa 2019 kabla ya kuanza kujenga barabara zingine'' Kindiki alisema.
Akiwa katika msafara huo aliweza kusimama katika soko la Mucatha Chuka eneo la Igamba Ng'ombe katika Kaunti ya Tharaka Nithi ili kuweza kuangalia jinsi utaratibu na mwendelezo wa ujenzi wa barabara ulivyokuwa ukiendelea wa kilomita 30 katika barabara ya Kibugua-Itugururu -Ishiara .
Mbunge wa eneo bunge la Igamba Ng'ombe bwana Patrick Munene alikuwepo katka msafara huo akiandamana na wananchi wa eneobunge hilo kwenye hafla hio ya kuendeleza maendeleo mashinani.
Shughuli hio inapoendelea Rais William Ruto anatarajiwa kuruzu katika eneo pana la Mlima Kenya kwa hafla ya ziara ya kuzindua miradi mbalimbali katika eneo hilo.
Hata hivyo watu wengi wanasubiri kushuhudia kuona jinsi rais atakavyokaribishwwa katika eneo zima la Mlima Kenya ambalo limei bukia kuwa ngome hasimu kwake licha ya kupata kura nyingi eneo hilo .
Rais William Ruto amekuwa akiwatema viongozi kutoka eneo hilo na ambao wana ushawishi mkubwa na ambao wawiliweza kumsaidia kujinyakulia ushindi karika uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2022.
Aliyekuwa naibu wa rais enzi zile Rigathi Gachagua aliweza kubanduliwa mamlakani na mabunge yote mawili mwaka jana huku akisalia kuwa kijana wa mtaani kule Mlima Kenya huku KITHURE KINDIKI akichukua nafasi yake.
Kiongozi wa hivi karibuni aliyeweza kutemwa na rais kutoka eneo hilo la Mlima Kenya ni aliyekuwa waziri wa utumishi waa Umma bwana Justine Muturi ambapo nafasi yake iliweza kuchukuliwa na mbunge wa mbeere Geoffrey Kiringa Ruku.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!