caption
Mwanadada mkenya Shorn Arwa sasa anafichua mbinu alizotumia kuwadanganya watu wa familia yake ili apate pesa za kutosha ili kumuezesha kusafiri nchini Dubai akiwa na lengo la kupata mume huko.

Shorn Arwa amesisitiza kwamba ilimulazimu adai kwamba anaenda katika shughuli za kimasomo ili wanafamilia waweze kumuchangia fedha.

Ameeleza kwamba aliamua kwenda Dubai ili kutimiza tamaa yake ya kupata mume huko. Anazungumzia safari yake huko na alivyofaulu kuingiliana na maisha yale.

'Sisemi wanaume wa Kenya ni wabaya lakini wakati nilikutana na mume wa Duibai mambo yalienda vizuri. Nilitoka Kenya nikiwa na lengo la kuenda kutafuta mume Dubai wala sio boyfriend," alieleza.

"Niliambia ndungu yangu kwamba kuna project ya shule nataka unichangie, na hiyo ikaongeza nauli yangu ya kwenda Dubai. Nilisema naenda kusoma kuhusu saikolojia na wakanichangia. Nilijiambia naenda holyday Dubai na naenda kutafuta bwana," alieleza zaidi.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Mwanadada huyo pia amesisitiza kwamba alifurahishwa sana na wazazi wa mumewe pamoja na familia yake. Akieleza kwamba walimfanyia vitu ambavyo si vya kawaida hapa Kenya.

"Wao ni tofauti sana na sisi. Mwanzo hawana utamaduni kama wetu. Huko ukishajifungua wanakuosha, wanakuchoma na maji moto, Mama mkwe au dada ya mume wangu ndio anafanya hiyo kazi. Nilioshwa kwa mwezi mmoja nikasema sasa mniache nimemisi kuoga mwenyewe,' alifichua kuhusu maisha ya Dubai.

Ameendelea na kueleza kwamba jambo ambalo alishangazwa sana nalo ni kuhusu chakula chao. Alieleza kwamba alilazimika kula chura na konokono ila baadaye alizoea na hicho ni chakula cha kawaida huko.

"Huko vitu tofauti sana ni vyakula, Nilikula chura,  konokono na dudu kamasi, na wanajua kupika, wanapika vizuri, wanaweka pilipili. Konokono ni tamu sana na napenda. Huko wavuvi wanaenda kuvua chura na wanauza. Chura ikishakarangwa inaonja vizuri kama samaki," alisisitiza.

Shorn Arwa alieleza kwamba mara ya kwanza hakujua kama amekula chura na alipogundua hilo alikosa amani kwa muda baadaya akagundua ni chakula cha kawaida.

'Niliuliza hii ni nini inakaa tamu ivo, nikaambiwa ni chura. Nilikasirika lakini tayari nishakula na ni tamu, na kila mtu anakula, hakukua na la kufanya," aliweka wazi.