Peter Salasya

MBUNGE wa Mumias Mashariki, Peter Salasya ameendeleza manung’uniko yake kufuatia kushambuliwa Jumapili iliyopita katika uwanja wa Nyayo alipojitokeza kusherehekea mechi.

Salasya aliungana na wakenya wengine wengi waliojitoeza katika uga wa Nyayo kushabikia timu ya taifa ya Kenya ilipokuwa inachuana na Gabon katika mechi ya kufuzu kombe la dunia, 2026.

Hata hivyo, baada ya kufika, mbunge huyo ambaye amekuwa mwiba mchungu kwa kumshambulia Raila Odinga alishambuliwa vikali hadi ikawalazimu maafisa wa polisi kumuokoa na kumsindikiza hadi kwa gari lake nak uondoka.

Mbunge huyo sasa anadai kwamba amewasamehe waliomtendea madhira hayo, lakini akaonesha mashtaka juu ya maisha ya watu hao.

Kwa mujibu wa Salasya, japo amewasamehe waliomshambulia, lakini ana wasiwasi huenda Mungu akaamua kuwaadhibu kwa kukatisha maisha yao, kwani ni kawaida kwa yeyote anayemfanyia unyama hadi kulia, kufa baadae.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

“Nimewasamehe wale wahuni wa ODM na sichukui hatua zozote za kisheria dhidi yao, lakini tatizo ni Mungu anaweza kuamua kuwaondoa kwa sababu yeyote anayenigusa na nilie huwa anakufa,” Salasya alisema.

Akizungumza kwenye video iliyowekwa kwenye akaunti yake ya X siku ya Jumatatu, Salasya alisema kuwa waliohusika na tukio hilo walijua kuwa atahudhuria mchezo huo na walitumia fursa hiyo.

“Kilichotokea jana (Jumapili) kilikuwa ni kitu kilichopangwa, nakumbuka mimi ndiye niliyekuwa wa kwanza kuwaambia watu waje Nyayo.

Salasya alieleza kuwa ameiacha timu yake ya ulinzi nyuma akiamini kuwa soka inawaunganisha Wakenya na atakuwa salama. Alisimulia jinsi alivyoonywa getini baada ya kufika lakini akaelekea kwenye kiti chake.

"Wakati naingia (uwanja), ilipangwa na kuna mtu alinionya getini. Kisha kuna kijana mmoja alikuwa akinifuata kila mahali nilipokwenda, nilipanda hadi VIP na bado alikuwa akinifuata," alisema.

 

Alishikilia kuwa washambuliaji waliratibiwa, na vitendo vyao havikuwa vya bahati nasibu.

"Ningeweza kuamua kwenda kuketi katikati ya uwanja na mchezo huo ungeahirishwa. Chaguo jingine lingeweza kusababisha mkanyagano," Salasya aliongeza.