Killed 
Kisa cha kushangaza kimetokea katika kaunti ya Wajir ambapo msichana wa miaka 17 ameuliwa na mwili wake kuchomwa moto kukiwa na madai kwamba alikataa kuolewa na mwanaume wa miaka 55.

Tukio hili ambalo limeangaziwa na runinga moja hapa nchini limetokea katika kambi ya wakimbizi ya Daadab hapa Kenya linaweka wazi masaibu ambayo watoto wa kike hupitia. 

Inasemekana familia yake ambayo ni ya wakimbizi kutokea nchini Somalia ilimlazimishwa mwanadada huyo kuolewa kwa lazima jambo ambalo alikataa na baadaye akuliwa na familia ya aliyepangiwa kuwa mumewe.

Msichana huyo kabla ya kifo chake alifichua kwa mama yake mzazi kwamba maisha yake yalikuwa hatharini kupitia mtandao wa whatsapp ila hakufaulu kupata usaidizi.

Mimi napigwa saa 24, huyu sio mwanaume. Nilisalitiwa kuolewa kwa huyu mwanaume. Angalia vile uso wangu umechanika. Sina mwanaume hapa. Anapata uungwaji mkono wako kila wakati. Hakuna mtu anataka kunisikiliza, kila wakati ninapoingia kwa nyumba hiyo napigwa," alizungumzia msichana huyo kupitia mtandao wa whatsapp kabla ya kifo chake.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Mama ya msichana huyo kwa upande wake alielezea jumbe alizopokea kutoka kwa familia ya alitakiwa kuwa mume wa mtoto wake wakielezea kwamba hatawahi kumuona mwanawe tena.

Aliendelea na kufichua kwamba anafahamu majina ya watu wote ambao wamehusika katika kitendo hicho cha ukatili kwa mwanawe.

"Usiku wa saa nne wakati watu walikua wanatoka kuswali,  Alinipigia simu akisema wameanza kunichinja, na simu yangu inataka kuchukuliwa. Ilipofika sa nane za asubuhi nilipokea simu nyingine. Wakaniambiwa msichana wangu amechinjwa na mwili wake ukaekwa kwenye matress na ukachomwa," alieleza mzazi huyo, "Kisu kimepatika kwenye eneo la tukio."

"Mtu ambaye alikuwa amemuoa na ndiye alimuua anaitwa Mohammed Kassim Tifo. Mwanaume ambaye alichukua simu yake anaitwa Musa Tifo Kasim maana alinipigia jioni iliyopita na akaniambia huyu msichana hatawahi rudi tena kwenye kambi ya wakimbizi, sababu hamna haja ya wewe kumuona tena," Alifichua mwanamke huyo ambaye ni mzazi wa msichana.

Mwaka wa 2022 shirika la utafiti duniani liliwahi kuandika kwamba zaidi ya watu milioni mbili wanaishi katika ndoa za kulazimishwa.