
GEORGINA Njenga ameweka wazi masharti yake katika ndoa ikiwa atalazimika kuingia katika ndoa tena.
Hii ni baada ya ndoa yake na mpenziwe Tyler Mbaya maarufu Baha Machachari kusambaratika takribani miaka miwili iliyopita.
Akizungumza na Morin Actress, Njenga alisema kwamba ushauri pekee anaoweza kuwapa wapenzi wachanga kuhusu kufungua akaunti za YouTube ni kwamba wafanye hivyo kwa ajili ya hela na wala si kufurahisha wat utu bure.
Alisema kwamba yeye kwa sasa hivi kila kitu anakifanya kwa ajili ya pesa na haswa katika masharti ya kimkataba, akisema hata ndoa sasa hivi anaiangalia kimkataba zaidi.
Alisema kwamba yeye akitaka kuolewa tena, atafanya kwa masharti ya mkataba kama wa miezi 6 hivi ili kupima maji na unga kama ikishindikana kila mtu anaenda zake.
“Mimi ningeshauri wanandoa wachanga kuanzisha akaunti za YouTube kwa sababu ya pesa na pia kwa ajili ya kujenga familia. Lakini usimzalie kwanza wewe kama mrembo, usiharakishe kufanya huo uamuzi,” Njenga alisema.
“Mimi hata natamani ningeweza kurudi pale nyuma niifanye kwa ajili ya pesa. Mnaweza hata ingia katika mkataba na mpenzi wako. Sababu mwisho wa siku ifikirie kama biashara…juu hata mimi sasa hivi nikieza olewa naolewa kwa mkataba,” aliongeza.
“Naanza na miezi 6 tukiona hatuwezani ni sawa, na kama tutawezana tunaongezea miaka 2,” Njenga alisema huku akisisitiza kwamba ndoto zake za kuolewa bado hazijafifia kabisa lakini akaweka wazi kwamba hayuko tayari kwa ndoa kwa sasa.
Awali, mama huyo wa mtoto mmoja alikiri kwamba kuna wakati mwingine huwa anajuta kuachana na mpenzi wake akisema kwamba sababu ambazo zilifanya wao kutengana hazikustahili kuwa kubwa hadi kufikia hatua hiyo.
“Hata haikuwa sababu ya msingi sana, nilikuja kuifikiria (baadae) ni kama ilikuwa ya msingi kidogo lakini kwa sasa kusema ukweli kuna wakati mwingine mimi hujuta kuondoka. Kwa sababu mitaani kuna baridi. Lakini majuto ni kama 2%,” Njenga aliongeza.
Kuhusu kilichomuuma zaidi katika harakati ya kutengana kwake na Tyler Mbaya, Georgina Njenga alisema kwamba aliumia zaidi kuona familia ikisambaratika kuliko kuona penzi likimwagika.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!