Baada ya zoezi la kuwahoji wawaniaji katika nafasi ya mwenyekiti kukamilika hapo Jumatano 26 Machi,2025 sasa ni awamu ya kuwatafuta makamishina wa tume ya IEBC.
Mchakato huo uliong'oa nanga leo tarehe 27 Machi,2025 na utakamilika tarehe 25 Aprili,2025 ambapo jumla ya wawaniaji 105 watahojiwa na tume iliyoundwa kwa ajili ya kuwapiga msasa.
Zoezi hilo ambalo huwa linaendeshwa katika jumba la bima mtaa wa South C likiongozwa na mwenyekiti Nelson Makanda linatarajiwa kufanya kazi ya ziada kwa makamishina hao ambao wameratibiwa katika siku tofauti tofauti.
Jopo hilo la kuwahoji makamishina hao lilisema kuwa wakenya wanastahili kuwa na imani kwa kuwa zoezi hilo linaendeshwa kwa haki, usawa na uwazi bila mapendeleo wala mwegemeo wowote.
Makamishina ambao wameratibiwa kuanza kuhojiwa leo ni Abduba Mollu Ido kutoka Isiolo,Abdihafid Abdullahi Yarrow kutoka Wajir,Abdihakim Adan Abdi(Wajir), Abdi Maalim Hussein(Mandera), Abraham Kipruto Langat(Nakuru) na Adhan Nuri Berhe( Tana River).
Itakumbukwa wazi kwa siku tatu zilizopita kulikuwa na mchakato wa kumtafuta mwenyekiti wa tume ya IEBC ambapo jumla ya wagombeaji kumi na mmoja waliweza kuhojiwa waliohojiwa katika nafasi ya uwenyekiti ni Erastus Edung, Ethekon,Francis Kakai Kisinger,Jacob Ngwele Muvengei, Joy Brenda Masinde Mdivo,Lilian Wanjiku Manegene,Robert Akumu Asembo,Sauli Simiyu,Abdulqadir Lotfi, Ann Atieno Amadi na Charles Ayako Nyachae.
Hata hivyo zoezi hilo linapoendelae wakenya wengi wameonekana kuwa na imanii vilevile kuonyesha utulivu huku wakiaachia asasi hiyo uhuru wa kutekeleza wajibu wake wa kisheria hadi wakati mwafaka ambapo mbivu na mbichi itabainika.
Jumla ya majina tisa yatawasilishwa kwa Rais na tume baada ya kukamilisha usaili ambapo rais atawateuwa makamishina saba ambao watafanya kazi kwa pamoja na mwenyekiti wa tume vilevile na kikosi cha sekrirtari ili kufanikisha mpango mzima wa uchaguzi.
Itakumbukwa wazi kuwa tangu mwisho wa uchaguzi uliopita tume haijakuwepo hivyo kuna chaguzi mbalimbali ambazo hazijaandaliwa kutoka maeneo mbalimbali ya taifa huku wakaazi wa eneo hizo zikikosa uwakilishaji bora na sawa ukilinganisha na sehemu ambazo zina wabunge na madiwani husika
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!