Jounalist
Wanahabari wapatao saba wametiwa mbaroni kwa kosa la kuangazia maandamano ambayo yamekuwa yakiendea nchini humo kwa siku sita mfululizo kufikia sasa.

Wanahabari ambao wamekamatwa  wameshtakiwa kwa kosa la kushiriki katika mikutano na maandamano haramu. Zaidi ya watu wapatao 1,000 pia wamekamatwa wakati wa ukandamizaji wa maandamano dhidi ya serikali.

Machafuko ya wenyewe kwa wenyewe nchini humo yalizuka baada ya meya Istanbul Ekrem Imamoglu, mpinzani mkuu wa kisiasa wa Rais Recep Tayyip Erdogan, kukamatwa kwa mashtaka ya ufisadi wiki iliyopita.

Waandishi wa habari walishtakiwa kwa "kushiriki katika mikutano na maandamano haramu," ingawa watetezi wa haki walisema wanahabari  hakuwa sehemu ya maandamano lakini walifanya kazi yao tu kama wandishi wa habari.

"Kufungwa kwao hakukubaliki. Hii ndio sababu ninakuomba uingilie kati haraka iwezekanavyo ili kupata kuachiliwa haraka kwa wandishi wa habari," Mkurugenzi Mtendaji na mwenyekiti wa AFP Fabrice Fries alisema katika barua kwa rais wa Uturuki, katika karipio kali kutoka kwa shirika la habari lenye makao yake mjini Paris.

Maelfu ya watu waliandamana, wakielekea makao makuu ya manispaa ya wilaya hiyo, wakitaka serikali ijiuzulu.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Waandamanaji walipeperusha bendera na mabango yenye kauli mbiu zilizosomeka "Tayyip jiuzulu!" huku watu katika vyumba vya juu wakigonga sufuria kuunga mkono.

Kuhusiana na kukamatwa kwa Imamoglu, serikali ya Uturuki imekataa madai ya ushawishi wa kisiasa na inashikilia kuwa mahakama ya nchi hiyo ni huru na inafanya kazi yake

Rais Erdogan ameshutumu chama cha upinzani cha Republican People's Party (CHP) kwa kuwachochea raia, akiapa kwamba wataona aibu kwa "uovu" unaofanywa kwa nchi mara tu "onyesho" lao litakapofifia.

Akizungumza na kundi la vijana katika mlo wa kuvunja mfungo wa Ramadhani siku ya Jumanne, rais wa Uturuki alihimiza uvumilivu.

"Wale wanaotisha mitaa yetu na wanataka kugeuza nchi hii kuwa mahali pa machafuko hawana pa kwenda. Njia waliyochukua ni mwisho," Erdogan alisema.

Upinzani wa nchi umetangaza mkutano mkubwa wa kudai haki kwa wapinzani waliokamatwa siku ya Jumamosi

"Je, uko tayari kwa mkutano mkubwa katika uwanja mkubwa huko Istanbul siku ya Jumamosi kumuunga mkono Imamoglu, kupinga kukamatwa kwake, kudai kesi za uwazi, za wazi, kusema tumetosha na tunataka uchaguzi wa mapema?" Ozel ambaye ni mpinzani wa serikali aliwauliza waandamanaji kwenye mkutano wa hadhara Jumanne.