Khalif Kairo
Mfanyabiashara wa magari ya jijini Nairobi Joseph Kairo Wambui maarufu Khalif Kairo ambaye amekua akiandamwa na kesi baada ya mteja wake kumshitaki kwa kukosa kukamilisha makubaliano.

Kairo alifikishwa mahakamani na mteja wake na  kushtakiwa kwa kutumia hila za ulaghai katika jitihada za kuwashawishi wateja wake kumtumia pesa za kuagiza magari ambayo anadaiwa hakuwahi kuwasilisha.

Kesi hiyo imekuwa ikiendelea na mahakama imeamuru mwanabiashara huyo kulipa dhamana ya shilingi milioni mbili kwa wakati mmoja la sivyo abakie rumande wakati kesi yake ikiendelea kusikilzwa.

Khairo ameeleza kwamba anajaribu awezavyo kusuluhisha mambo ila vyombo vya usalama vinamwandama kila wakati. Ameeleza kwamba kwa sasa bondi aliyopewa na mahakama hana uwezo wa kupata  kwa hivyo ataelekea kukaa rumande.

"Najaribu sana kuweka mambo yawe sawa kwa kusuluhisha ila polisi wanaendelea kuniudhi na kusambaratisha mazungumzo. Kwa sasa sitakuwa na uwezo ya kupata shiliingi milioni mbili, ni rumande kwa sasa," aliandika mfanyibiashara huyo.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Hata hivyo ameelezea imani yake kwamba mwenyezi Mungu atamusaidia kutoka kwa masaibu yanayomwandama. Amewataka watu kumuombea.

Tutajenga upya, na mwenyezi Mungu atatusaidia kupita kwa hili. Kuanzia sasa sitakuwa kwa mtandao. Nawapenda na muendelee kuniombea," ujumbe wake ulisomeka kupitia mtandao wa X.

Awali Kairo alifikishwa mbele ya Hakimu Mkuu Lucas Onyina na kukanusha mashtaka hayo.

Kulingana na hati ya mashtaka, Kairo kwa tarehe tofauti kati ya Julai 10, 2024, na Julai 25, 2024, huko Westlands kwa njia ya hila za ulaghai alimshawishi Jeff Munane kumlipa Sh2.1m.

Pesa hizo zinadaiwa kulipwa kwake kupitia kampuni yake ya Kai&Kairo Limited.

Ilikuwa kwa ajili ya uagizaji wa mseto wa Honda Vezel kutoka Japani, ambayo karatasi ya mashtaka zilioonyesha hakuwahi kuwasilisha.

 Inadaiwa alifanya kosa sawia dhidi ya Dona Okoth. Hati ya mashtaka inadai kuwa Dona alituma Sh2.98 milioni kwenye akaunti ya benki ya KCB ya Kai na Kairo Limited. Hizi ni baadhi ya kesi zinazomwandama Kairo.