Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna 

Seneta wa Nairobi na katibu mkuu wa chama cha ODM Edwin Sifuna aliweza kuelezea wasiwasi wake na jopo linalowapiga msasa wawaniaji wa nafasi ya uwenyekiti wa IEBC.

Sifuna aliweza kusema kuwa alikuwa na tashwishi kubwa na namna jopo linavyoendesha mchakato huo mzima kwa wawaniaji waliofika katika jopo hilo la kuwapiga msasa kwa kuwasaili. 

''Sina uhakika na kile ambacho jopo hili linatafuta kwa hawa wawaniaji, wanajopo wana maswali mengi kwa wagombeaji ambayo yanaonekana kutosaidia kuleta suluhisho na kwa kumpata mwenyekiti ambaye anaafikia kiwango cha kuwa mwenyekiti''. Sifuna alisema.

Kwa upande mwingine Seneta wa Narok Ledama Olekina  aliweza kutoridhia majina ya wagombeaji waliofika katika jopo la usaili kwa kuyasawri majina hayo kama majina ambayo tayari yalishawahi kuwa katika afisi za serikali kwa namna moja au nyingine.

Olekina alielezea kutoridhiswa kwake na majina hayo kwa kuyataja kama majina ambayo yamebadilishwa kutoka nafasi moja ya kazi hadi nyingine.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

''Mimi ninaamini kuwa si vizuri tena ni vibaya kwa orodha ya majina ya wagombeaji wa mwenyekiti wa IEBC ambaye atawezesha kulisukuma taifa katika viwango  vingine vikuu siku za usoni hasahasa likikuja kwa swala hili la uchaguzi . Haya majina ya wawaniaji ni majina ambayo yametolewa katika nafasi za kazi nyingine za awali, ni wakati mwafaka tupate kiongozi kijana mwanaume  mchanga ambaye ataendesha tume hii kwa manufaa makubwa''. Olekina alisema.

Baadhi ya orodha ya  majina ya wawaniaji wa kujaza nafasi hii ya tume ya uchaguzi na mipaka IEBC katika nafasi ya mwenyekiti ni aliyekuwa msajii wa mahakama Ann Amadi, Charles Nyachae,Abdulqadir Lorot,Jacob Ngwele,Joy Mdivo,Edward Katama,Kakai Kissinger,Erastus Ethekon,Robert Akumu,Lilian Wanjiku na Saul Simiyu.

Jopo hilo lilianza kuwapiga msasa wagombeaji hawa mnamo siku ya Jumatatu 24,2025   na litaendelea hadi siku Jumatano 26, Machi 2025 ambapo baada ya  kila mmoja kukamisha kupigwa msasa jopo litateua majina ya wawaniaji wawili ambayo yatapelekwa kwa rais na mmoja wao atachaguliwa kama mwenyekiti wa tume.

Jumatano ndio siku ya mwisho ya kuwapiga msasa wawaniaji hao wote  hatimaye jopo zima likiongozwa na Mwenyekiti wao Nelson Makanda watatoa taarifa na kuelezea jinsi mchakato ulivyokuwa hadi kufikia kiwango cha kuwateua wawaniaji bora.