Rais William Ruto mesema kwamba Waziri wa utumishi wa umma na ambaye pia alikuwa mwanasheria mkuu wa serikali Justine Muturi alikuwa hawezi kazi katika enzi zake.
Rais alipokuwa akiwahutubia waisalamu katika ikulu ya Nairobi siku ya Jumanne 25 Machi ,2025 katika hafla ya sherehe za ifutari Rais alikuwa akijibu swali ambalo jamii hiyo ilikuwa imerai serikali kuwezesha fedha za kuanzisha wakfu Pamoja na kuidhinishwa rasmi katika dini hiyo.
Katika jawabu lake Rais Ruto aliweza kusema kuwa ombi walilokuwa wamependekeza litekelezwe kwa jamii ya waislamu lilikuwa linataka liweze kutolewa kwa kutiwa sahihi na mshauri mkuu wa serikali kama njia mojawapo ya hitaji la Kisheria.
Rais aliwaomba radhi kwa kusema kuwa mpango huo ulicheleweshwa kwa sababu aliyestahili kutekeleza wajibu huo kama kiongozi alikuwa hana uwezo wa kutekeleza kazi vyema.
‘’Tunapoendelea kusonga mbele kwa kuangazia masuala ya elimu jinsi ambavyo mmesema na vilevile kuangazia suala kuu la kuhusu kupata wakfu kwa hakika ni jambo ambalo limekawia sana kwa kuchukua muda mrefu ila mniwie radhi kwa hilo kwa sababu nilikuwa na mshauri mkuu wa serikali ambaye alikuwa hajui kazi ipasavyo lakini kwa sasa nina mwanadada ambaye anachapa kazi kwa uzuri hivyo tutatekeleza’’.Rais Ruto alisema.
Mzozo kati ya Waziri wa utumishi wa umma bwana Muturi na serikali ulianza tu pale ambapo kulishuhudiwa maandamano ya vijana wa kizazi cha Gen Z mwaka jana Juni wakati ambapo kulishuhudiwa maandamano ya kupinga mswada wa Fedha wa 2024/2025.
Katika kipindi hicho kulieza kushuhudiwa vijana wengi wakitekwa nyara ili kuweza kutuliza hali tete iliyokuwepo enzi hizo na katika harakati hizo mtoto wa aliyekuwa mshauri mkuu wa serikali na ambaye ni Waziri wa utumishi wa umma kwa sasa Justine Muturi aliweza kutekwa nyara.
Miezi sita baadaye Bwana Muturi alijitokeza katika vyombo vya Habari na kuanza kuikashifu serikali kwa kuweza kuwa katika njama ya kumteka mwanawe pasi sababu zozote wala kumuwasilisha mahakamani kwa makosa ya kutekwa nyara.
Tangu hapo kumekuwa kukishuhudiwa vita vya maneno baina ya Waziri Muturi na serikali huku akiwa mstari wa mbele kulaani tabia inayoendeshwa na serikali pasi kuwaajibisha wahusika wa utekaji nyara.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!