
MCHEKESAHI na muigizaji, Eunice Mammito ametaka jumbe za kumhongera kwa kupata mtoto kutumwa kwake kwa njia ya miamala ya pesa.
Mama huyo mpya mjini alichapisha picha akiwa amempakata mwanawe mchanga na kusema kwamba angependa wale wanaompa hongera kwa kuwa mama kufanya hivyo kupitia jumbe za M-Pesa pekee.
Mammito alichapisha nambari ya till kwa ajili ya kufanikisha miamala hiyo, akiashiria kwamba jumbe tupu za kumhongera hazina athari kwake na ndio maana angependa kuhisi hongera za dhati kupitia kupokea pesa.
“Jumbe za hongera zikuje kwa njia ya M-Pesa,” Mammito aliandika huku akifuatisha na nambari ya Till.
Takwa hili linajiri saa chache tu baada ya mrembo huyo kufichua kuwa yeye ni mama mpya, japo hakuweka wazi jinsi ya mwanawe.

Mammito alifichua kuwa mjamzito mwaka jana wakati wa Maandamano ya vijana wa Gen Z akisema kwamba alihisi ni wakati mwafaka kwake.
Akizugumza kwa mara ya kwanza kuhusu ujauzito wake Desemba mwaka jana, Mammito alidinda kufichua mhusika, lakini akasema kwamba mimba yake hakununua ila asingependa kufichua utambulisho wa mhusika.
“Hii mimba yangu sijanunua, ni ya mtu tu; ni kijana tu wa watu na ni mtoto wa mtu Fulani,” Mammito alieleza.
Kuhusu ni kwa nini hayuko tayari kumtambulisha mhusika huyo kwa mashabiki wake mtandaoni, Mammito alisema kuwa anafanya hivyo ili kumkinga yeye na pia mwanawe kutoka kwa hukumu hasi za watu wa mitandaoni.
‘Lazima wafichwe hii Nairobi. Huwezi jua. Useme ndio huyu waseme ooh hakai vizuri na wengine wamchukue na mimi sasa hivi nina umri wa miaka 31, sitaki kuanza kuuliza mtu eti rangi uipendayo ni gani, katika huu umri nimeshakua sasa, unaelewa,” Mammito alifafanua.
Katika mahojiano hayo na runinga ya TV47, Mammito pia alikanusha tetesi kwamba mhusika alikuwa mpenzi wake wa zamani, Eddie Butita na kusema baba wa mwanawe mtarajiwa alikuwa mtu asiye maarufu mitandaoni.
“Mimi na Butita ni maneno ya kale, ni muda mrefu uliopita kama miaka 4 iliyopita. Kwa huyu, ni mtu ambaye si maarufu mitandaoni. Na nafikiri mtu wa aina hiyo ndiye nilikuwa nataka, mwenye anajishughulisha na mambo tofauti kabisa na tasnia yetu ya mitandaoni.”
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!