
KIONGOZI wa chama cha upinzani cha NUP nchini Uganda, Bobi Wine amekubali mwaliko wa mkuu wa majeshi Muhoozi Kainerugaba ambaye ni mwanawe rais Museveni la kutaka wapigane.
Kainerugaba, ambaye amekuwa akionyesha waziwazi chuki yake dhidi yam wanasiasa huyo alitoa wito kwake akimtaka kumjaribu katika mduara wa vita ikiwa kweli anaona atammudu.
Muhoozi, ambaye kwa sasa ameifunga akaunti yake ya X, alisema kwamba kwa vile Bobi Wine amekuwa akidai kuwa shabiki na mpenzi mkubwa wa mchezo wa ngumi, basi amjaribu yeye katika pambano moja.
“Anasema anapenda mchezo wa masumbwi, basi namwalika kwa pambano la ngumi,” Muhoozi Kainerugaba alichapisha.
Bobi Wine kwa ujasiri alimjibu akitanguliza na Kauli ya kijasiri kwamba amekubali mwaliko huo huku akimtaka Kainerugaba kutangaza tarehe na na yeye atatangaza sehemu ya kufanyika kwa mchuano wao.
Hata hivyo, Bobi Wine alikubali pambano hilo kwa masharti kwa mkuu huyo wa majeshi akisema kwamba ikiwa Muhoozi atamshinda basi yuko radhi kuachana na siasa kabisa.
Pia, Wine alisema kwamba sharti lingine kwa Muhoozi ni kukubali kuacha pombe ikiwe atamshinda katika pambano hilo.
“Nimekubali mwaliko kwa pambano. Kama utanishinda nitaachana kabisa na siasa, lakini kama nitakushinda itabidi umeachana na pombe. Sema ni lini na mimi nitasema ni wapi,” Bobi Wine alisema.
Muhoozi amekuwa akichapisha jumbe la kutishia maisha ya Bobi Wine, mara nyingi akimrejelea kwa jina la utani la ‘Kabobi’.
Mwezi Januari mwaka huu, Kainerugaba alichapisha ujumbe wa kutaka kumuadhibu Bobi Wine, akisema kwamba mtu pekee anayezuia adhabu hiyo kufanyika ni baba yake, rais Yoweri Museveni.
Ni ujumbe ambao uliibua wasiwasi ya Bobi Wine ambaye alisema kwamba jaspo ulionekana kuwa wa utani lakini ulikuwa unahusishwa na kutamatisha maisha yake huku akimkashifu Muhoozi kwa kutumia mamlaka yake visivyo.
“Kabobi anajua kwamba mtu pekee anayemlinda kutoka kwangu ni babangu. Kama mzee wangu hangekuwa, ningekata kichwa chake leo,” Muhoozi aliandika.
“Tishio la mtoto wa Museveni (ambaye pia anaongoza jeshi la Uganda) la kunikata kichwa si jambo ninalolichukulia kirahisi, ikizingatiwa kwamba wengi wameuawa na yeye na baba yake, na kwa kuzingatia majaribio yao kadhaa ya kuniua. NIKATAA kutishwa na utawala waoga. Ulimwengu unatazama,” Wine alijibu akinukuu chapisho hilo la Kainerugaba.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!