
SOSHOLAITI Vera Sidika amefichua baadhi ya dhana potovu ambazo watu wanazo dhidi yake, haswa kuhusu urembo.
Akizungumza kwenye podikasti ya mwanablogu wa Nigeria Afolasade Samagbeyi, Sidika alifichua kwamba idadi kubwa ya watu wanadhani kwamba hana lingine lolote la kutoa zaidi ya kiuno chake kipana.
Mama huyo wa watoto 2 alisema kwamba watu wengi hudhania kwamba yeye ni zuzu asiye na akili licha ya kubarikiwa na mwili mzuri lakini akakanusha akisema kwamba wale ambao wamekutana naye wanamjua kama mtu mwenye akili nyingi ajabu.
“Watu wanadhani kwamba ooh Vera ako na kiuno kipana…ni kama hicho ndicho kitu pekee anacho. Watu wengi kwenye akili zao wanadhani kwamba hicho ndicho kitu pekee ninaweza kuwa nacho.”
“Watu huwa hawafikirii kwamba kunaweza kuwa na mengi ya ziada kwa huyu mrembo. Watu ambao wako karibu na mimi ndio wanamjua Vera wa ukweli na hicho ni kitu ambacho siwezi nikasimama nikimthibitishia kila mtu.”
“Kwa bahati mbaya wengi wanadhani kwamba mimi nina makalio makubwa bila akili lakini ukweli ni kwamba mimi ni mahiri sana acha nikwambie,” Vera Sidika alijieleza.
Kuhusu uhalali wa kiuno chake kipana, Vera Sidika alisisitiza kwamba ni halisi na asili kabisa akisema hujawahi fanya upasuaji hata mara moja.
“Unadhani niliwahi kufanya BBL? Hapana! Huu mwili wangu ni asili kabisa. Nahisi kwamba sababu inayowafanya watu kudhani kwamba nilifanya BBL ni kutokana na kuna wakati nilifanya picha ya utani mitandaoni ambayo nilihariri na kukata kabisa makalio yangu nikidanganya kwamba nilipatwa na dharura ya kimatibabu.”
“Mwili wangu ni asili kabisa na hata unaweza gusa,” aliongeza.
Mrembo huyo alisema kwamba jambo kuu analojivunia zaidi katika maisha yake mpaka sasa ni uamuzi wa kuwa mama kwa malaika wawili – Asia Brown na Ice Brown.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!