
SIKU chache baada ya Zuwena Platnumz kudai kwamba atamkwapua msanii chipukizi wa Kenya, Nexxie na kumpeleka Tanzania ili kumkuza kimuziki, mchekeshaji wa humu nchini, Dj Shiti naye amekariri kwamba kipaji cha msanii huyo ni kikubwa ajabu.
Katika video ambayo inaenezwa mitandaoni, DJ Shiti alirekodi video akifurahia moja ya ngoma za Nexxie Music na kutabiri kwamba chipukizi huyo akiendelea kwa kasi hiyo, huenda akawavuruga sana wasanii wakubwa Kenya.
Kwa mujibu wa Shiti, Nexxie Music ana fursa nzuri ya kujikweza na kuwa uso mpya wa muziki wa Kenya, haswa baada ya wengi wa wasanii tegemezi kuonekana kulegeza kamba na kupunguza kasi katika kuachia miziki ya kuwakosha mashabiki wa Kenya.
Shiti alisema kuwa msanii huyo ana sauti nzuri, utunzi mzuri na wa kipekee ambao unaleta ladha halisi ya Kikenya kwenye masikio ya wapenzi wa muziki.
“Anaitwa Nexxie Music msanii chipukizi kabisa kutoka +254, huyu anaenda kusumbua sana sanaa ya muziki. Talanta tupu kutoka Kenya. Nexxie hii nimeweka tiki,” Dj Shiti alisema katika video hiyo.
Ungamo la Shiti kuhusu ubora wa chipukizi huyo linajiri wakati ambapo mrembo aliyepata umaarufu baada ya kucheza kama pambo kwenye video ya Zuwena ya Diamond Platnumz kuwasuta Wakenya, akisema kuwa wangekuwa wanajua kuwashika machipukizi wao mikono, basi Nexxie angekuwa miongoni mwa majina makubwa.
Mrembo huyo alitishia kumchukua Tanzania na kumsimamia kimuziki huku akiwatahadharisha Wakenya dhidi ya kukurupuka kuwa ni wao wakati nyota yake itakapong’aa.
“Wakenya wanapenda kuongea sana lakini kupigana support hawawezi. Kitu kidogo wanapakini, mbona mnapaniki Kenya, mbona? Wakenya mnajua kuongea sana lakini hamwezi ku’support wenzenu,” alitupa jiwe kwa Wakenya.
“Mimi nataka nimchukue huyu Nexxie nimlete Tanzania nimsimamie kimuziki ila akijak ufikia kiwango Fulani wasije kudai kwamba ooh ni msanii wetu wakijibvunia. Hawawezi jivunia kwa sababu mimi nitakuwa nimembadilisha kuwa wa huku,” aliongeza.
Nexxie Music ni moja kati ya majina ya ajabu yaliyoteka maskio ya wapenzi wa muziki nchini Kenya tangi mwaka jana.
Msanii huyo kwa sasa anatamba na kibao chake cha ‘We Hafi Do It’ ambacho kilitoka takribani wiki mbili zilizopita.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!