Crime scene

Shabiki mmoja wa mpira alilalama baada ya gari lake kuibiwa kutoka  mahali alikokuwa  ameliegesha.

Mlalamishi alisema kuwa  alikuwa ameliegesha gari lake kando ya barabara  ya Kisauni nyuma ya hospitali ya Nairobi, alipokuwa akitazama mechi Kati ya Harambe star na Gabon ugani Nyayo.

 Aliporipoti  katika kituo cha Polisi cha  AKILA mlalamishi aliweza kusema kuwa aliegesha gari lake IST lenye nambari ya usajili KBN 093B lenye rangi  ya shaba  saa 3:40pm na akafululiza hadi kwenye uwanja kulipokuwa na mashabiki wa kushabikia mchuano wa  soka.

Akisimulia masaibu yake ya kupoteza  gari vilevile na timu ya taifa Harambee star kupoteza  kwa kupigwa mabao mawili kwa moja baada ya mchezaji Aubameyang kuwaweka Gabon Kifua mbele kwa magolo 2-1, alisema jioni ya saa moja alirudi kulichukua gari lake akapata haliko.

Baada ya kuwasilisha stakabadhi zote na kuonyesha kuwa gari lili,opotea lilikuwa lake, gari hilo limeweza kutangazwa kote kama gari lililoibiwa na maafisa wa DCI kutoka kituo cha Langata  hivyo kuruhusu msako mkali dhidi yake.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Kwingineko katika eneo la  JuJa uchunguzi wa kina unaendelea kutafuta aina  mojawapo ya Gari lililoibiwa   TOYOTA AXIO lenye Usajili  KCR 628U ambalo liliibiwa  kutoka mtaa wa Matangi karibu na shule ya msingi ya Kimbo.

Mwenye gari alikuwa ameliegesha gari hilo   katika mahali pake pa maegesho mtaani ila alipoamukia asubuhi hakulipata wala kuliona jambo ambalo lilimuacha akiwa amechanganyikiwa na akiwa na msongo wa mawazo.

DCI iliweka  wazi nambari za mawasiliano ili kuweza kusaidia katika shughuli ya uchungiuzi na kupatikana kwa magari hayo yote yalioyoibiwa , nambari ya kupigaripoti kwa polisi ni 999911112 au 0800722203 ikitumia kauli kuwa Fichua kwa DCI.

Kulingana na DCI uchunguzi wa kina unalengwa kuanzishwa ili kuhakikisha kuwa magari hayo yanapatikana na walioyaiba wanakamatwa na kufunguliwa mashitaka kulinganna  na mjibu wa  sheria , hata hivyo umma umeibua hali ya wasiwasi kutokana na ripoti nyingi za wizi wa magari kila uchao hio ikiashiria kuwa wanancghi wengi wataanza kuhofia kuegesha magari katika maegesho ya umma kwa sababu ya ukosefu wa usalama wa kutosha.