Jopo  lililotwikwa jukumu la kutathimini na kumteua mwenyekiti wa IEBC litaanza shughuli ya kuwahoji wagombeaji leo Machi 24,2025.

Katika taarifa kwenye vyombo vya  Habari siku ya Jumapili 23,Machi 2025,  iliratibiwaa kuwa shughuli ya kuwapiga msasa wagombeaji wa kutafuta nafasi ya  mwenyekiti wa IEBC itaanza Machi 24,2025 saa mbili ambapo zoezi hilo litaendelea kwa muda wa siku tatu mtawalia na kutamatika Machi 26,2025.

Mwenyekiti wa jopo la kamati bwana Nelson Makanda alisema kuwa  jopo mwanzoni lilikuwa limechapisha idadi ya watu 11 katika vyombo vya  habari na katika  mtandao  wa wavuti wa  Bunge la taifa mnamo Machi 14,2025.

‘’Jopo la la wanachama wa kumteua mwenyekiti wa  IEBC na makamishina wengine wa tume hiyo wana furaha kutangazia umma kuwa mchakato wa kuwahoji wawaniaji hao katika nafasi ya mwenyekiti wa IEBC utaanza rasmi mnamo Machi 24,2025 kuanzia saa  mbili unusu asubuhi’’ bwana Makanda alisema.

‘’ Kwa kuongezea jinsi ilivyochapishwa  katika magazeti ya  taifa gazeti la Daily Nation na gazeti la the Standard na katika mtandao wa wavuti wa bunge la  taifa Ijumaa Machi 14,2025 jumla ya wagombeaji 11 watahojiwa kwa siku tatu  ambaopo zoezi hilo linatarajiwa kukamilika tarehe 26 Machi,2025’’.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Wagombeaji walishauriwa kuwasilisha sitakabadhi sahihi ikiwemo barua kutoka kwa afisi ya mkurugenzi mkuu wa upelelezi na makosa ya jinai DCI, Bodi kuu ya kutoa mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu,taasisi ya ukusanyaji ushuru KRA, Tume ya kupambana na ufisadi EACC  Pamoja na barua kutoka kwa bodi kuu inayosajili  vyuo  vikuu vyote nchini CUE.

Hata hivyo wananchi waliombwa kuwasilisha malalamishi yoyote kwa  jopo siku tano kabla ya siku ya mgombeaji huyo kufika ili kuweza kuwasilisha dukuduku zake dhidi ya mgombeaji ili tume ipate  wakati mwafaka wa kutathimini madai ya malalamishi,aidha tume ilisema  lalamishi hilo liambatane  na  hati kiapo ya barua iliyo katika  njia ya maandishi.

Umma uliweza kuombwa kuwasilisha malalamishi yao au shauku dhidi ya wagombeaji walioteuliwa kwa kutuma nakala fifi kwa barua pepe [email protected]o.ke 

Zaidi ya hayo, kamati hio  ilihakikishia umma kuwa zoezi hilo litakuwa la haki ,wazi na la kuaminika.

‘’Tungepenga kuchukua fursa hii kuwapongeza enyi vyombo vya Habari kwa  kuwa mstari wa mbele kuangazia zoezi hili kuanzia mwanzo wa uundaji wa jopo hadi ku kufikia sasa hamashisheni umma kila kitu kinachojiri hapa’’. Mwenyekiti wa Jopo alisema. 

Miongoni mwa wanachama  ambao wanagombea nafasi hiyo ni aliyekuwa mwenyekiti wa jopo lililounda Katiba ya 2010 Bwana Charles Nyachae na aliyekuwa msajili wa mahakama Bi Ann Amadi miongoni mwa wengine .