Evaline Muthoka, Gospel Artist
Mwanamziki wa injili kutoka hapa nchini Kenya Evaline Muthoka ameeleza wazi safari yake ya unyanyapaa kutoka na masaibu ya vifo yaliyokuwa yamekitiri katika familia yao.

Muthoka amefichua laana ambazo zilikuwa za majonzi makubwa kwa familia yao akieleza kwamba licha ya kuzaliwa wasichana sita ni yeye pekee  ambaye yuko hai kwa sasa.

Jambo ambolo ni la kuhuzunisha zaidi ni kwamba dada zake walikuwa wanaaga dunia wakati wako kwenye ndoa na na baada ya maafa yao siku chache bwana zao pia walikuwa wanawafwata.

"Wasichana watano wote wameega dunia na kila anayekufa anafatana na mume wake isipokuwa mmoja ambaye aliaga pekee yake. Mimi nishawai pewa talaka kotini kwa sababu niko na laana ya kifo. Nilikataliwa mbele ya watu kwa sababu ya kifo na kwetu kulikuwa kunaitwa makaburini," alieleza Muthoka kwa uchungu.

'Ndugu zangu na wake wao wawili, baba yangu na mama yangu, dada zangu wawili pia wakazikwa hapo nyumbani, ndugu yangu mwingine ambaye hakuwa ameoa pia akazikwa hapo. Kwetu kulikuwa kunaitwa makaburini," alifichua msani huyo.

Mwanamuziki huyo wa injili akisimulia machungu ya kupewa talaka na mumuwe ambaye alikuwa amemuuoa baada ya kujua kwamba kwao watu walkuwa wanakufaa wakifuatana jambo ambalo ni kumbukumbu akilini mwake mpaka leo.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

"Baada ya madada zangu wawili wa mwisho kufa, na yule aliyenioa akanikataa, akasema nimebeba laana ya kifo. Dada zangu wakikufa wanakufa na bwana zao na hayuko tayari kufa. Sasa wakati nilibaki pekee yangu akaniambia ukitoka kwa mazishi rudi kwenu. Akasema hayuko tayari kuishi na mtu ambaye amebeba laana ya kifo," alisimulia mwanadada Muthoka.

Mwanamziki huyo amesimulia kwamba kamwe watu wa familia walipozidi kuondoka duniani ndipo masaibu yalipozidi kwani walikuwa wanamuachia watoto wao ambao watu waliogopa kuishi nao kwa kuogopa mikosi ya vifo.

"Hapo ndipo maisha yangu yaliharibika, watoto 17 wamebaki, kila anayekufa anaacha watoto," alieleza

Mwanamziki Muthoka hata hivyo ameeleza wakati alipata mwanga wakati akiwa anaimba kwenye kongamano na hapo ndipo alipatana na  mume ambaye alisimama naye kwenye maombi na anaishi na yeye mpaka leo.

"Siku moja baada ya miaka mingi ya hivyo vifo, Nilikuwa naimba kwa hisia, kumbe mzee Muthoka  aliyekuwa amekuja kama 'Camera man' akaniona kama mke wake. lakini kidogo akasikia watu wakisema huyu msichana amebeba laana ya vifo," alisema.

Muthoka ameeleza mwanaume huyo alimpenda, wakafanya harusi na anaishi na yeye mpaka leo. Amempongeza kwa kumushika mukono na kurejesha matumaini katika maisha yake na vifo visivyo vya kawaida vimekoma katika familia yao.