DCI waliwakamata washukiwa wawili wa ulanguzi wa dawa za kulevya na mihadarati.
Katika operesheni ambayo iliendeshwa dhidi ya kukomesha na kunasa dawa za kulevya kama vile nikotini,usafirishaji na uuzaji wa dawa hizo.
Kikosi kizima cha kupambana na Mateja kwa ushirikianao na maafisa wa polisi kutoka kituo cha polisi cha Mugutha na maafisa wa halimashauri ya polisi NGAO waliwakamata wasafirishaji wawili wa dawa hizo Pamoja na misokoto ya bangi 800.
Mshukiwa wa Kwanza ambaye ana umri wa miaka 30, mwengine wa miaka 21 walikamatwa wakiwa na misokoto hiyo katika mtaa wa Kimbo.
Maafisa hao hawakunasa tu misokoto bali waliweza kupata hata bangi iliyokuwa katika Sacheti mbalimbali,Sacheti 13 zenye uzani wa giramu 35 kwa kila moja ilihali sacheti tano zilikuwa na uzani wa giramu 130 huku sacheti 44 zikiwa na uzani wa giramu 16 mtawalia.
Hata hivyo kuliwezwa kunaswa mashine mawili ya kidigitali katika operesheni hiyo ambayo iliashiria kuwa ilikuwa ni opereshini iliokuwa imepangwa kwa ustadi na kwa mtindo maalum.
Washukiwa hao wako katika kituo cha polisi ambapo uchunguzi wa kina unaendelezwa na maafisa wa polisi kuwahusu ipasavyo kabla ya wawili hao kufikishwa mahakamani.
Katika maeneo ya Moyale mafisa wa kitengo cha kupiga doria waliweza kuikamata pikipiki yenye nambari ya usajili KMGM 369D ikiwa imebeba magunia mawili yaliyoshukiwa kutokana na kile kilichokuwa ndani huku mwendeshaji akitoroka na kuacha gari hilo barabarani.
Kwa kuweza kufanya msako na uchunguzi maafisa wa polisi waliweza kupata ndani vifurushi 20 vya bangi ambapo ilikuwa na uzani wa kilo 100 ambapo pikipiki Pamoja na dawa hizo ziko mikononi mwa polisi ambapo zimehifadhiwa kama Ushahidi.
Hata uchunguzi wa kina unaendelea ili kuweza kuwapata na kuwakamata washukiwaa hao waliopatikana na dawa hizo amb po baada ya hapo wataweza kushitakiwa kulingana na mjibu wa sheria.
Visa vya watu kupatikana wakisafirisha bangi na bidhaa za magendo zimekuwa zikiripotiwa katika sehemu mbalimbali za jamuhuri ya Kenya huku wito kutoka kwa Idara ya usalama ikizitaka taasisi za usalama kukaza mkono ili kuwakamata wahusika.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!