Seneta maalum Gloria Orwoba alifanikiwa kupata nafasi ya kurudi katika bunge la Seneti baada ya kususia kusoma msamaha jinsi alivyotakiwa kufanya.
Siku ya Alihamisi Machi 20,2025 Orwoba aliitikia wito wa kusoma msamaha alioandikwa na bunge la Seneti baada ya bunge la Seneti kususia msamaha aliokuwa amejiandikia mwanzoni.
Katika msamaha wake Orwoba alikubali makosa na kuomba msamaha kwa kile alikuwa amekitekeleza katika kikao cha kuanza.
‘’Mimi Seneta Gloria Orwoba ninaapa kwa kuomba msamaha kwa bunge la Seneti , Maseneta ,Karani wa Seneti na Makatibu wote wa Seneti kwa kujihusisha na kuonyesha tabia mbovu.Kulingana na Kifungu cha Katiba nambari 16(e) aya ya saba na nane ya awamu ya nne ya nguvu za bunge ambazo zina fursa na ambazo zinaakisi pakubwa kuhusu maadili ya bunge kwa wanachama wake ilikuwa kinyume na matakwa ya bunge na wanachama wake’’ . Hati ya msamaha ilieleza.
‘’Ninasema kuwa nitawajibika na kuheshimu majukumu ya uongozi jinsi ambavyo imeelezwa katika Katiba kuhusu uongozi na maadili katika kifungu nambari 2012 cha nguvu za bunge na fursa za kifungu 2017 kwa hivyo ninaomba kukurudishwa katika vikao vya bunge ninawashukuru’’.Orwoba alisoma.
Mnano siku ya Jumanne ,Machi 18,2025 Bi Orwoba alizuumu kuondoka katika vikao vya bunge baada ya kususia kusoma msamaha alioandikiwa .
Mbunge ambaye kwa muda wa siku 70 alitakiwa kuwa kwenye likizo ya lazima ambayo iliratibiwa kuwa ingeisha Mei 1, 2025 ilibatilishwa na kuwa siku 30. Baada ya hapo aliweza kuitwa ili asome msamaha aliokuwa ameandikiwa kulingana na nguvu na mamlaka ya kamati naya Pamoja ilivyoamuru katika Seneti ila akaamua kusoma msamaha wake binafsi.
Hatimaye baada ya Spika Kingi kubaini kuwa kulikuwa na maneno tofauti katika msamaha wake alimwamuru Orwoba kusoma msamaha aliokuwa ameandikiwa na seneti au atoke nje ya Seneti hadi wakati maalum atakaojisikia kuja kusoma msamaha ulioandikwa na Seneti.
Siku ya Jumatano Uongozi wa muungano wa Mawakili wa kike(FIDA- KENYA) waliweza kuelezea kutoridhishwa kwao na maamuzi ya bunge la Seneti kwa kutomkubalia Seneta Orwoba kusoma msamaha wake bali asome ule wa kuandikiwa FIDA ilifafanua kwa maelezo.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!