Ramadan
Waumini wa dini ya kiisilamu wanapoendelea na mfungo wa mwezi mtukufu wa ramadan Sheikh Yusuf Nasir ameeleza umuhimu wa kufunga na kusali zaidi katika siku kumi za mwisho.

Sheikh Nasr ameeleza wazi kwamba siku kumi za mwisho ni muhimu zaid kwenye mfungo kwani hapo imani yako imeinuka na mwenyezi Mungu husamehe.

"Kikubwa katika siku hizi kumi za mwisho, ni kwamba mwenyezi Mungu ametoa ruksa kubwa na nafasi kubwa kwa yeyote mwenye kudai ama kutaka kumuomba na yeye atamjibu. Kwa hivyo ni fursa ambayo mtume anasema tuitumie kwa sababu mwenyezi Mungu katika siku hizi huteremka na kuuliza nani mwenye jambo lake," alieleza Yusuf.

"Nani Mwenye kutaka kuniomba ili mimi nimjibu. Waisilamu tunaomba, maanake sote tuna matatizo. Sote tuna vilio, sote tuna jambo la kumuomba mwenyezi Mungu," alieleza zaidi.

Akizungumza pia amewataka waisilamu kutumia muda wa usiku kusali zaidi ili kumuomba Mungu kama alivyofunza mtume.

"Katika mambo yetu mengi tuchukue nafasi hizi za usiku. Ambazo tunaambiwa kwamba akiweza mtu atumie usiku wote, na asipoweza atumie nusu yake, na asipoweza atumie hata robo yake. Ilimradi kwamba aitumie kumuomba Mungu jambo la kwanza, alafu pili kufanya mambo ya heri," alieleza zaidi."Mwenyezi Mungu ametuhimiza tufanye mema katika siku hizi, ili kwamba katika mema tupewe ziada ndo maana husali usiku." 

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Kwenye mafunzo na maelezo Sheikh Nasir afafanua kwamba wakati wa Usiku mwenyezi Mungu husamehe. Na msamaha wa dhambi unatokana mtu kuswali mbele za Mwenyezi Mungu.

"Mwisho kuna msamaha wa dhambi  hiyo pia inatoka na mtu kuhuisha sala zae za usiku. Atakapokuwa ameswali atasamehewa. Kama alivyotufunza mtume kutufundisha katika hadithi yake kwamba Mwenye kusimama kisimamo cha kusali usiku  katika ramadhani Mwenyezi Mungu atamsamehe.