Waziri wa usalama wa ndani Kipchumba Murkomen alimhakikishia mamake mvulana aliyetoweka kwa jina Brian Odhiambo kuwa haki itapatikana.
Alipokuwa akizungumza naye Bi Elizabeth Auma mkaazi wa Nakuru, mnamo Jumatano Machi 19,2025 ambapo alimhakikishai kuwa haki itapatikana kwa jamaa na familia ya Brian aliyetoweka katika ziwa Nakuru.
‘’Nikirudi Nairobi nitaketi na wale ambao walikuwa wanafanya uchunguzi waniambie uchunguzi ulifikia wapi? Lakini nia yangu ni kuhakikisha kuwa mwishowe umepata haki .Nitalichukulia hili suala kama langu ila chenye ninaweza sema tu ni kuwa pole kwako na kwa jamii yako ila haki itapatikana’’ Murkomen alisema.
Hilo lilitokea baada ya Bi Auma kukatiza hotuba ya Murkomen alipokuwa kule Shabab Nakuru Magharibi katika hafla ya kuzindua kampeni ya kitaifa ya watu kujisajili kupata vitambulisho vya taifa.
Murkomen aliweza kuwaamuru maafisa wake wa usalama kumuruhusu aseme naye hio ni baada ya kushangiliwa na umati wa watu kwa ujasiri huo alioonyesha. Baadaye Waziri aliweza kumwalika Bi Auma katika afisi za halimashauri ya Kaunti ili aeleze kwa kina kilichojiri kuhusu mwanawe.
Auma alimurai Waziri aweze kumsaidia kupata kule mwili wa mwanawe ulipo,alimurai Waziri kwa masikitiko makubwa.
‘’Maafisa wote waliohusika katikla tukio hilo watafikishwa kortini na watapoteza kazi zao. Kuna wakenya wengi waliotoweka kama Brian ni mamake tu Brian ambaye amenifikia na kunitarifu kuhusu kutoweka kwa mwanawe, ningependa kuwaarifu kuwa niko imara na wewe na nitafanya kila juhudi kuhakikisha kuwa wale maafisa wa KWS waliohusika watatuambia Brian yuko wapi’’ Waziri Murkomen alisema.
‘’Tumeshuhudia baadhi ya maafisa wa KWS wakihusika katika biashara ya uuzaji Samaki ndani ya ziwa Nakuru wakati ambapo wakenya wengine wanapokuja kufanya shughuli za biashara hapo wanateswa na kunyanyaswa na maafisa hao’’ Waziri alieleza.
Brian Odhiambo aliripotiwa kupotea mnamo tarehe 18 Januari,2025 akiwa karibu na kampuni ya KWS upande wa ziwa Nakuru alipoonekana mwisho.
Baada ya juma moja mahakama ya Nakuru iliamuru afisa msimamizi wa mbuga ya wanyamapori ya Nakuru atoe mwili wa Brian akiwa hai au maiti.
Mnamo Jumanne Machi 18,2025 Wakili wa familia ya Odhiambo na wanaharakati waliruhusiwa ndani ya mbuga ambapo walikisia kuwa mwili wa Brian ulikuwa umezikwa na hivyo haungeonekana.
‘’Makaburi yote yanaonekana yamechimbuliwa na miili kutolewa ila nina uhakika na matumaini
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!