Winner of Ballon d'Or
Mchezaji wa Real Madrid Kylian Mbappe ameonyesha mshangao wake kuona kiungo wa kati wa Manchester City Rodri akishinda Ballon d'Or ya 2024 mbele ya mchezaji mwenzake wa Real Madrid Vinicius Junior.

Vinicius ndiye aliyependwa zaidi kutwaa tuzo ya kifahari zaidi ya soka, na maafisa wa Madrid walishangazwa sana na uamuzi wa kumkabidhi Rodri tuzo hiyo hivi kwamba walisusia hafla nzima.

Katika mahojiano na vyombo vya habari Mbappe aliulizwa kuhusu nafasi ya mshambulizi  wa Paris Saint-Germain Ousmane Dembele kushinda Ballon d'Or mwaka huu, na akasema ushindi wa Rodri unamaanisha kuwa chochote kinawezekana katika mbio za tuzo.

"Mchezaji wa Ballon d'Or ni nini? Rodri, yeye ni mchezaji wa Ballon d'Or kwako?" alianza. "Kwangu mimi, mwanzoni, hakuwa mmoja, nilifikiri Ballon d'Or ingeenda kwa Vinicius lakini mwishowe, ni Rodri aliyeipata.

"Ikiwa ningekuambia hivyo miezi mitatu iliyopita, ungeniambia, 'Unazungumza nini?'.

"Leo, hatujui Ballon d'Or itaenda kwa nani, isipokuwa kwamba hakuna mtu anayepaswa kutengwa, kwamba wachezaji wote wanaweza kutuzwa, wakati mwingine hata kipa." alisema Mbape.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Kabla ya ushindi wa hivi karibuni wa Real Madrid dhidi ya City katika mechi za mchujo za Ligi ya Mabingwa Ulaya, kocha Carlo Ancelotti alisisitiza kuwa walikuwa sahihi kususia sherehe ya Ballon d'Or kwa kumuunga mkono Vinicius.

"Sidhani kama ulikuwa uamuzi mbaya," Ancelotti alisisitiza. "Hatukutaka kushiriki kwa sababu tulidhani kwamba Vinicius alikuwa sahihi kuwa mshindi wa Ballon d'Or.


"Na hii haimaanishi kuwa hatuna heshima kwa Rodri aliyeshinda Ballon d'Or kwa sababu ni mchezaji mzuri. Lakini nadhani tulifikiri, na nilifikiri, kwamba Rodri alistahili kushinda mwaka uliotangulia, 2023," aleleza Carlo Ancelotti, mkufunzi wa Real Madrid.