Kanisa  la Katoliki laendeleza wito  wa kupinga michango ya pesa nyingi makanisani na wanasiasa kutoka matabaka mbalimbali.

Kiongozi na Mwenyekiti wa Maasikofu dhebu la Katoliki katika jimbo la Kisumu Askofu Maurice Muhatia aliweza kusema kuwa mara nyingi kanisa lilitegemea michango mbalimbali kutoka kwa washiriki  wao jambo ambalo lilikuwa la manufa kwa pande zote mbili ila akasema kuwa michango hiyo iliweza kufanyika kwa usiri pasi kutangazwa kiasi cha fedha.

‘’Tangu zamani hata enzi ya mtakatifu mwana wa Maria Yesu Kristo kanisa lilitegemea michango mblimbali jambo ambalo lilisaidia sana kuimarika kwa kanisa’’ Askofu alisema

Alisema kuwa mara  nyingi ukitaka kumusaidia au kuchangia mtu ni vyema kufanya kwa unyamavu na usiri pasi kutangaza bali si kuambia  kila mtu  mahali eti umemppa msaada au mchango wa kitu Fulani.

Maurice Muhatia Makumba mwenyekiti wa Maasikofu wote aliweza kusema kuwa kama kanisa wako mstari wa mbele kupinga na kupigana na ufisadi katika kila pembe ya Jamhuri ya Kenya.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Kiongozi huyo wa dini aliweza kutoa taarifa ya kuongoza wanadini wote na viongozi wa dhehebu hilo mada ambayo kila kanisa la katoliki litachukua juma hili kwa kuwahutubia wafuasi wao katika misa itakayoendeshwa kanisani ujumbe mkuu ukiwa ni kupambana na kupinga ufisadi.

Aliweza kusisitiza akisema kuwa ni wajibu wao kama kanisa na viongozi kwa jumla kupigana na ufisadi kwa hali na mali wakizingatia zile athari ambazo ufisadi huweza kuleta katika jamii na kwa Wakenya kwa jumla.

Uongozi na usimamizi wa kanisa la Katoliki unajitokeza wazi kuweza kutangaza msimamo wake dhidi ya  michango na harambe kanisani ikiwa imezua tumbo joto kuhusu uhalali wa pesa za wanasiasa ambao hutoa pesa nyingi makanisani.

Itakumbukwa kwa siku za hivi karibuni viongozi mbalimbali wa siasa akiwemo rais wa nchi wameonekana pakubwa kuzuru sehemu na makanisa mbalimbali wakitoa michango ya kila aina katika makanisa mbaliamabali kwa kutoa michango ya mamilioni ya pesa.

Kutokana na michango hio ya pesa nyingi zinazotolewa na viongozi katika makanisa jambo hilo  limechochea hasira ya wananchi wakitaka kujua ni wapi hela hizo nyingi hutoka ikikusudiwa kuwa kuna maswala muhimu nchini kama sekta ya afya, elimu na usafiri ambazo zinakumbwa  na changamoto kadhaa ikiwemo gharama ya Maisha.

Wananchi wengi wamekuwa wakirai makanisa mbalimabli kutowakubali wanasiasa makanisani wakisema kuwa wanatumia pesa za umma kuwadhulumu raia kwa kutoa michango huku wakitelekeza wajibu wa kuangazia maendeleo na miradi muhimu kwa jamii na badala yake kuzidisha michango ya mara kwa mara.