Junet Mohamed ambaye pia ni mbunge wa Suna Mashariki alidai kuwa jamii ya Kiislamu itakuwa na athari kubwa kuamua mshindi wa uchaguzi ujao wa 2027.

Alisema hayo alipokuwa katika sherehe za maankuli maalumu ya chakula cha IFTAR mtaa wa Upper Hill Siku ya  Jumatano Machi 19,2025.

‘’Sisi kama Waislamu tuko ngangari. Katika nchi  yetu sasa tuko wengi. Uchaguzi huu unaokuja, muislamu atakuja kusema yote. Kwa sababu kura ya waislamu sasa ni kura nyingi sana katika taifa hili,” Junet alisema.

Junet alizungumzia ukubwa wa jamii ya Kiislamu akiitaja kuwa jamii kubwa nchini ambayo ina kura nyingi sana katika Jamuhuri tukufu ya Kenya hivyo akitaja umoja wa jamii hio kama utakaokuwa  na athari ya maamuzi katika uchaguzi wa mwaka wa 2027 akiashiria kuwa kuna uwezekano hata jamii hio kukuwa na nafasi ya kusimamisha rais kivyake.

’Na hapa mbele, kuna watu watasimama Urais ama Naibu wa Rais. Kura za Waislamu ni nyingi na haitachukuliwa hivihivi. Tutaweka vitu kwa meza na watu watahesabu. Kuna wengine wanafikiria wako wengi kushinda wengine, lakini ngoja kura zipigwe waone ni kina nani ni wengi,” Mbunge huyo wa Suna Mashariki alisema.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Alipokuwa akizungumza aliweza kumrai na kumwalika Waziri mkuu wa zamani bwana Raila Odinga ambaye alikuwa katika hafla hiyo ili aweze kusilimu na achukue dini ya kiislamu kwa maana amekuwa na mchango mkubwa katika jamii hio.

‘’Upendo wako kwa waislamu unajulikana. Ni upendo wa dhati na ni upendo ambao umekuwa kwa muda mrefu sana. Tunakuombea Mungu akujalie uwe muislamu na ufuturu na sisi Ramadhan ijayo ukiwa kama muislamu,” kiongozi wa waliowachache bungeni alidadavua kwa ustaarabu .

Matukio hayo yalijiri wakati ambapo bwana Odinga alisema kuwa alikuwa ameisoma kurani yote na alifahamu sheria nyingi za kiislamu katika muongozo unaotolewa na Kurani.

Baadhi ya sheria tano ambazo ni nguzo muhimu katika uislamu ambazo bwana Odinga aliweza kusema ni kama kumtambua ALLAH kama Mungu mkuu,kumtambua nabii MOHAMED,Kufanya maombi mara tano kwa siku ukitazama MEKA, Kuwapa misaada wasiojiweza,kufunga wakati wa Ramadhani na kutimiza amri hizo ambazo ni nguzo muhimu sana.