Huduma ya kitaifa kwa polisi(NPS) ilitoa na kuelezea mikakati ya usalama ambayo imewekwa kufuatia mashindanao ya WRC Safari Rally 2025 ambayo yanang;oa nanga Alhamisi ya tarehe 20/03/2025 hadi Jumapili 23/03/2025 mjini Naivasha.
Katika ujumbe wake kwa mtandao wa X huduma ya polisi iliweza kuwarai wananchi kuzingatia masharti yote ambayo yamewekwa pamoja na kushirikiana na polisi kufanikisha usalama wa kila mmoja.
Baadhi ya maagizo yaliyotolewa na huduma ya kitafa kwa polisi ni matumizi ya barabara mbadala ambazo umma utaambiwa kuelezewa kuzitumia vilevile kuwepo kwa maafisa wa trafiki katika Barabara zote ili kuhakikisha kuwa kuna usafiri mwema bila matata.
Hata hivyo huduma hiyo ya polisi ilisema kuwa kwa ushirikiano na huduma ya kitaifa ya usafiri barabarani (NTSA) itahakikisha kuwa kila kitu kinaendeshwa jinsi kilivyoratibiwa pasi shida yoyote.
Huduma hiyo iliweza kushauri umma kuzinggatia maagizo na utaratibu wote uliowekwa na asasi za kiusalama na kushauri umma kuripoti visa vyovyote vinavyotishia usalama wa wananchi.
Madereva wa mabasi na malori waliweza kushauriwa kutoegesha magari yao kando ya Barabara kuu ya Naivasha- Nakuru kwa ajili ya kutotatiza usalama mwema, watumizi wa Barabara kwa njia ya kusari kwa miguu na pikipiki pia waliombwa wawe wangalifu zaidi.
Huduma hiyo kwa polisi iliweza kutoa nambari za simu kwa umma na kutangaza wazi kuwa iwapo kunaweza kutokea jambo lisilo la kawaida au kutaka kuarifu umma bila shaka nambari za simu zilikuwa wazi kama ifuatavyo, nambari ya polisi bila malipo ni 099911112 au Fichu na DIC 0800722203.
Kando na usalama pia mashindano hayo hayazungumzii tu burudani pekee bali pia ni kitega Uchumi kikuu kwa wakaazi wa eneo la Naivasha na viunga vyake Pamoja na serikali kwa jumla kwani Mashindano hayo yataweza kuwavutia watalii wengi nchini ambao wataleta fedha nyingi kwa taifa.
Vilevile mikahawa mbalimbali na wafanyakazi watakaofanya kazi katika hoteli mbalimbali watanufaika na kujenga viwango vyao vya kimapato.
Mashindano ya Safari rally huweza kuwavutia takribani wageni elfu 100,000 na hutazamwa na watu katika vyombo vya Habari milioni 120 katika jumla ya mataifa 170 duniani na zaidi ya runinga 50 za kimataifa ambazo hupeperusha hewani mashindano hayo.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!