Betty Kyallo, Charlie Jones

CHARLIE Jones, kijana Gen Z ambaye ni mpenzi wa mwanahabari wa runinga ya TV 47, Betty Kyallo ameibuka kwa mara nyingine na dai la kujinyenyekeza kwa mama huyo wa binti mmoja.

Jones bila kuona aibu alipeleka kwenye instgram yake kueleza jinsi penzi lake na Betty Kyallo limekolea munyu kiasi kwamba kuachana ni ndoto ya alinacha.

Alifichua kwamba kila siku anaporauka asubuhi, jambo la kwamba analojikumbusha na kushukuru ni kwamba ni mmoja kati ya vijana wachache wenye wanawake warembo.

Pia alidai kwamba yeye yuko radhi kutii kila amri ya Betty Kyallo, akijitaja kama mbwa mtiifu ambaye atabweka mpaka kukuche ikiwa mmiliki wake (Kyallo) ataamrisha hivyo.

Pia alisema kwamba yuko tayari leo-kesho kufasnya chochote ambacho Kyallo atamtaka kufanya, ikiwa ni pamoja na kufanya shughuli za ndani hadi kuchota maji.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

"Ni asubuhi nyingine nijikumbushe kuwa nilipata mke motomoto. Mimi ni mbwa wake Akisema enda chota ninachota Anasema kubweka? Nitabweka woof woof woof hadi mtaa mzima uamke," Charlie alieleza.

Ujumbe wa Charlie Jones

Haya yanajiri siku chache baada ya Charlie kuyeyusha mioyo na ujumbe wa siku ya kuzaliwa kwa Betty alipofikisha miaka 36 Jumamosi, Machi 15, 2025.

Katika heshima yake, alimtaja kama moyo wake, amani yake, na baraka zake kuu.

"Sijui hata nianzie wapi kwa sababu maneno hayatawahi kutosha kuelezea jinsi ninavyokupenda. Wewe ni moyo wangu, amani yangu, baraka yangu kubwa. Wewe ndiye mtu wa kuchekesha zaidi ninayemjua- ndio, mcheshi zaidi kuliko mimi (nitakubali mara moja tu). Jinsi unavyochukia sana, kunifanya nicheke hata wakati sitaki, ni jambo la kushangaza kuhusu wewe. Kama, unaonekanaje mzuri hata kwenye pyjamas, sio sawa,” alisema.

Ujumbe huu ulikuja siku chache baada ya kijana huyo mdogo kuzua wasiwasi kwamba penzi lake na Kyallo liliporomoka.

Hata hivyo, katika kujieleza, alisema kwamba ujumbe huo ulishawishiwa na ulevi, akisisitiza kwamba yeye na Kyallo hawawezi kuachana kiboya.

Aliwageuzia mtutu wa mashambulizi wale ambao walionekana kusherehekea penzi lake na Kyallo kusambaratika, akisema kwamba aibu inasalia kwenye panda la nyuso zao.