Aliyekuwa Gavana wa Kiambu Ferdinand Waititu aliyehukumiwa kifungo cha miaka 12 gerezani au alipe kima cha shilingi milioni 53 kwa tuhuma za ufisadi kama faini.
Gavana huyo wa zamani wa kiambiu bila shaka alihiari kuenda mahakamani kurai apewe bondi huku akisubiri rufaa ya kesi yake kusikizwa na kuamuliwa.
Katika Jaribio la Pili wakili wake Kibe Mungai alisema kuwa kulingana na uhalisia wa mambo jinsi yalivyokuwa Bwana waititu alikuwa katika nafasi kuu ya kupata bondi kutokana na kesi ya dharura iliyowasiliswa Machi 11,2025 inayompa nafasi kuu bwana Waititu kupata bondi.
‘’Ombi la mshitakiwa la kukata rufaa lina nafasi nyingi za kisheria za kumpa mshitakiwa nafasi ya kufaulu katika kesi yake sehemu ya kesi ilieleza’’.
Mungai alisema kuwa kwa kuwa mteja wake tayari amekwisha hukumiwa itakuwa vyema na haki kwake kupewa bondi chini ya sheria za kifungu cha katika cha haki nambari 159(2).
Aliongezea kwa kusema kuwa haitakuwa haki kwa mteja wake kutumikia kifungu chake gerezani na vilevile rufaa yake ikose kufaulu haitakuwa haki kamwe.
Alifafanua kwa kusema kuwa mfungwa ana afua mbili katika kesi yake kulipa shilingi Milioni 53 jinsi ambavyo mahakama ilivyoamuru au kutumikia kifungu cha miaka 12 gerezani au kutoa dhamana ya kiasi sawa na hicho kuashiria kuwa mfungwa ana uamuzi wa kuamua cha kufanya.
‘’Kwa kuzingatia maelezo ya kisheria katika kifungu nambari 49(2) cha Katiba inakataza kufunga mtu jela kwa makosa aliyopatikana nayo kwa kumpa adhabu ya faini sehemu ya kifungu cha sheria ilieleza’’.
Vilevile Mungai aliweza kusema kuwa hapakukuwa na haja ya kumfungia mhusika ambaye ameathirika na ambaye anasubiri kusikizwa kwa rufaa yake mahakamani ili awe katika nafasi ya kuwa sawa kisheria.
Hata hivyo afisi ya mkurugenzi wa mashitaka ya umma DPP iliweza kurai mahakama kuipa siku tatu ili iweze kujibu madai kuwa waliweza kupokezwa barua ya kujibu mashitaka kwa kuchelewa.
Mahakama ya milimani iliweza kutoa uamuzi kupitia kwa jaji Lucy Njuguna siku ya Jumanne Machi 18,2025 iliweza kuipa siku tatu afisi ya ODPP kujibu ombi hilo.
Kesi hiyo itatajwa mnamo Machi 26, 2025 kudhibitisha iwapo kila hitaji liliafikiwa ipasavyo.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!