Gloria Orwoba, Nominated Senator
Seneta Gloria Orwoba ambaye aliteuliwa na chama kilichoko mamlakani UDA kuwakilisha akina mama katika bunge la seneti, alikuwa amereje bungeni jana Jumanne 18 Machi baada kuhudumia likizo yake ya lazima aliyopewa na bunge hilo.

Seneta huyo mteule baada ya kuwasili bungeni kama ilivyo adha alitakiwa kutoa hotuba ya kuomba msamaha kwa wabunge kwenye kikao chake cha kwanza.

Orwoba hata ivo alidinda kusoma maandishi yaliokuwa yameandikwa kama njia ya kuomba msamaha akidai huko kulikuwa kukiuka haki yake. Ameeleza haya kupitia mtandao wake wa facebook.

"Leo, nilikataliwa kuingia tena kwenye Seneti kwa sababu ya uamuzi wangu wa kutosoma msamaha nilioagizwa. Msamaha huu, kama ulivyo, unakiuka haki yangu ya msingi ya ulinzi dhidi ya kujibagua na kudhoofisha haki yangu ya mchakato wa haki," aliandika senata huyo.

Orwoba hata hivyo amesisitiza mwamba madai aliotoa kuhusu unyanyasaji wa kijinsia ambayo bado hayajachunguzwa hayamuruhusu kutoa tarifa zozote kutokana kwamba kesi hiyo bado iko mahakamani.

"Madai ya unyanyasaji wa kijinsia ambayo nimeyaibua bado hayajachunguzwa. Spika na Utawala wa Bunge wanafahamu kabisa kwamba nina mchakato wa mahakama unaoendelea, ambao utaathiriwa moja kwa moja na msamaha ulioamriwa. Kwa kunilazimisha nitoe msamaha nilioamriwa, seneti inanilazimisha kutoa taarifa za uongo ambazo zinaweza kutumika dhidi yangu katika mahakama kwenye kesi inayoendelea na baadaye," alieleza.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Mwanasiasa huyo ameomba msamaha kwa wabunge wenzake kwa kile alichokitaja kama kuchangia mtafaruku bungeni ila amekariri kwamba atasimama kidete kwa ukweli na haki na hataomba msamaha kwa kuzungumza kama mfichuaji.

"Ningependa kuchukua fursa hii kuwaomba radhi wenzangu kwa vitendo vyangu vyovyote ambavyo vinaweza kulileta Bunge katika hali ya kutoelewana. Hata hivyo, ninasimama imara katika kujitolea kwangu kwa ukweli na haki. Sitaomba msamaha kwa kuwa mwathirika au kwa kusema kama mfichua siri," aliendelea.

"Hii sio juu yangu tu, ni juu ya kuhakikisha kwamba hakuna mtu mwingine anayekabiliwa na mbinu kama hizo za vitisho na ukandamizaji. Ninaendelea kuwa imara katika harakati zangu za uwajibikaji na haki, na ninaamini kwamba haki itashinda,' alikamilisha maadishi yake.