Maafisa wa Polisi katika kituo cha polisi cha  Naivasha eneo la Naivasha walimkamata Jmshukiwa kwa kwa madai ya  kumiliki  silaha hatari kinyume  cha sheria.

Mshukiwa mwenye umri wa 30 alikamatwa na maafisa wa polisi kwa  madai ya kumiliki Bunduki iliyokuwa na marisasi mawili taarifa hizo ziliwafikia maafisa wa usalama kufuatia Habari kutoka kwa raia.

Wakishughulikia Habari hizo kwa njia ya dharura maafisa wa polisi waliari fiwa kuwa raia mmoja Aliona   mshukiwa mmoja  akiwa amebeba marisasi katika baa moja ya Nyama CHOMA kinamba Naivasha.

Maafisa wa usalama waliweza kuchukua hatua za upesi ili kubaini na kumkamata mshukiwa kutoka mahali aliposemekana alikuwa bila kupoteza muda wala kulimatia.

Kulingana na ukaguzi wa kina uliofanywa na maafisa wa usalama  wa kitengo cha DCI kuweza kutambua aina ya silaha ambazo mshukiwa alikuwa nazo ni kuwa  ilibainika wazi kuwa mshukiwa alikuwa anamiliki bunduki ambayo ilikuwa na urefu wa milimita 7.62 na urefu wa marisasi yenye milimita 9.

Mshukiwa alipatikana na silaha hizo haramu bila kuwa na vyeti au vibali vya kumruhusu kumiliki silaha hizo na  alikuwa anakusudia kufanya nini nazo? Maswali yaliulizwa yakimkosa majibu.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Mshukiwa baada ya kukamatwa alipelekwa   katika kituo cha polisi cha Naivasha ambapo uchunguzi wa kina unaendelea kumhusu mshukiwa  na baadaye ataweza kufikishwa mahakamani kujibu mashitaka baada ya uchunguzi kukamilika.

Maafisa wa DCI  kwa ushiriano na wananchi  mara nyingi wamekuwa macho na kuwahabarisha wananchi na kuwaarifu kuwa wawonapo jambo lolote ambalo si  sawa na ambalo linatishia usalama wa taifa au wananchi wawe tayari kupiga ripoti kwa  maafisa wa usalama  kwa kutumia nambri ya  simu  0800722203 bila malipo yoyote.

Kesi za  wananchi kupatikanabna silaha hatari bila vibali maalumu zimekuwa zikikithiri na kuchochea wasiwasi na uwoga kwa wananchi huku wanaopatikana na silaha hizo wakikosa kufafanuani wapi wanakopta silaha hizi haramu ambazo serikali instahili iwe na uwezo kwa kufahamu ni akina nani wanaomiliki silaha  hizo.

Juhudi za maafisa wa usalama kufanya bidii na juhudi za upesi kumkamata bwana Matu ni jambo ambalo linastahiki kupongezwa kwa dhati kuu ikizingatiwa kuwa kama mshukiwa huyo hangetambuliwa kutoka kwa wananchi angekuwa ni mwiba mkubwa sana kwa usalama wa wananchi kwa jumla.