Aliyekuwa Gavana wa Meru aliyebanduliwa Mamlakani Kawira Mwangaza alivunja kimya chake kwa mara ya kwanza tangu uamuzi wa korti ulipotolewa wa kumuondoa afisini.

Mnamo Ijumaa ya Machi ya tarehe 14,2025 mahakama kuu iliweza kuafikiana na uamuzi wa Seneti wa kumbandua  Mwangaza kama uliafikia viwango vyote vya Kisheria.

Akizungumzia hali yake ya kuondolewa mamlakani siku ya Jumanne ya tarehe 18 Machi,2025 kupitia kwa mtandao wake wa Facebook  Mwangaza aliweza kumtaja aliyekuwa Gavana wake Bwana Mutuma M’ethingia kama kibaraka mkuu na ambaye alitumika kufanikisha malengo ya mahasidi wake kisiasa.

Aidha aliweza kusema kuwa kuondolewa kwake kulichochewa na viongozi ambao ni wanasiasa wakuu walioshinikiza kubanduliwa kwake mamlakani.

Alisema kuwa kuondolewa kwake kulitokana na yeye kutokubaliana na viongozi madalali ambao walikuwa na azma ya kupora na kuvuja mali ya umma kwa njia ya ufisadi akisema kuwa yeye hakuwa  na wakati wa kuwapa sikio wala nafasi  hiyo hivyo walizuumu kumuendea bwana Mutuma ambaye  waliweza kumshawishi na kumtumia kama Daraja.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Aliweza kusema kuwa kutokana na msimamao wake mgumu wa kuhakikisha kuwa usawa, haki na sheria inafuatwa kwa kila jambo ni baadhi  ya sababu kuu zilizochochea maadui zake kumpiga vita kwani inasemekana walitaka mtu ambaye alikuwa wa kushawishika upesi.

Kwa upande mwingine viongozi walionekana wakimsifia Bwana Mutuma kwa kumtaja kama kiongozi ambaye kulingana na wao ni kiongozi ambaye hukaa afisini na kutia sahihi stakabadhi mbalimbali.

Kwa upande  mwingine Bi Kawira aliweza kutajwa kama kiongozi ambaye hakukuwa anachukua muda wake mwingi kukaa afisini wala kutia sahihi  stakabadhi mbalimbali bali alionekana akiwa mashinani kukagua na  kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo jambo ambalo halikuwafurahisha wengi.

‘’Ajenda kuu haikuwa kuhusu maendeleo na miradi ya Meru bali ilikuwa ni kuniondoa afisini kwa sababu wapinzani wangu walihisi nitawabwaga katika uchaguzi ujao wa 2027 kutokana na historia yangu ya maendeleo katika Kaunti hii ya Meru nimechapa kazi bila uwoga’’ Mwangaza alisema

Mwangaza kabla awe Gavana alikuwa mwakilishi wa kike wa Meru ambapo alianza kupalilia uongozi wake ifaavyo na akauchukua Ugavana wa Meru kama muaniaji Huru akiwabwaga washindani wake wa karibu Kama Kiraitu Murungi na Mithiika Linturi.