Aliyekuwa mwenyekiti wa kamati ya bajeti katika  Bunge la taifa Bwana Ndindi Nyoro katika mahojiano na vyombo vya Habari katika ukumbi wa KICC alisema hana kinyongo na mtu yeyote.

Katika mahojiano mbayo yalifanyka katika ukumbi wa KICC chumba nambari 26 Jumanne ya Tarehe 18 Machi,2025.

Bwana Nyoro aliweza kujitenga pakubwa na masuala ya siasa na badala yake akaweza kuutaja mkutano huo na mahojiano  hayo kama yaliolenga kuangazia masuala kuhusu nafasi yake kama alivyokuwa mwenyekiti wa kamati ya bajeti bungeni.

Akijieleza mwanzo kwa utangulizi Bwana Nyoro alielezea mwanzo faida kuu aliyopata kutokana na kuwa mwenyekiti wa Bajeti akisema iliweza kumpa uchu na ari ya kuweza kurudi vyuoni ili kujifunza zaidi kuhusu masuala na Uchumi,riba na mgao wa bajeti unavyooana kwa hatua moja na nyingine.

Aidha Nyoro aliweza kueleza kuwa kupitia nafasi hiyo aliweza kuelewa na kujifunza zaidi kuhusu jinsi mashirika mbalimbali ya serikali yanavyoshiriana ili kutoa huduma kwa wananchi  wa taifa lake.

Bwana Nyoro aliweza kuwashukuru Wakenya kwa kuwa wazalendo na kuweza kuamini utendakazi wake kwa kufanya kazi kwa moyo Mkunjufu na kwa kujitolea pasi kupokea lalama zozote kutoka kwa kamati yao ya wanachama 27 kulingana na maelezo ya bwana  Nyoro.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Vilevile bwana Nyoro aliweza kuelezea nafasi na fursa ambayo ataiweka katika kumbukumbu zake kwa wakati alipokuwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo akisema kuwa waliweza kuwashirikisha wakenya katika kupata maoni mbalimbli nchini.

Nyoro alisema kuwa waliweza kuzuru Magatuzi mbalimbali na jopo la kamati ili kuweza kupokea maoni ya ile miradi na masuala ambayo raia walikusudia yawe yakipewa kipaumbele ili bajeti ikipangwa inazingatiwa kulingana na maoni ya raia jambo ambalo ni hitaji mujhimu katika katiba jumla ya shilingi milioni 100 zilitengwa kufankisha hilo.

Bwana Nyoro vilevile aliweza kusema kuwa alijivunia sana walimu wa JSS kuandikwa na kuwa katika kandarasi ya kudumu.

Nyoro akijibu Maswali kutoka kwa wanahabari waliokuwa  na uchu na ari ya kumtaka atoboe siri na atangaze msimamo wake wa kisiasa, Mbunge huyo wa Kiharu alizima matumaini ya fikra hizo akisema kuwa hakukuwa na Kinyongo na mtu yeyote na hangeweza kusema masuala ya Siasa katika mahojiano hayo.

‘’Je katika kipindi chako cha uongozi kuna mtu yeyote kutoka kwa chama chenu aliwahi kukueleza kuwa kazi yako si Njema na ulihitajika kufanya mabadiliko’’? Mwanahabari mmoja aliuliza.

‘’La hasha hamna mtu wala kiongozi yeyote aliwahi nipigia simu wala kunishauri kuhusu kazi yangiu bwana Nyoro alijibu swali.

’Je, kufikia sasa ni kipi ambachho unajutia hukukifanya wakati ambapo ulikuwa mwenyekiti wa  kamati ya bajeti’’? Mwanahbari aliuliza Nyoro alisema kwa uchangamfu tena akasema kuwa hajutii kwani kila kitu alikitekeleza kwa wakati pasi kulimatia.

Kujibu swali kuhusu shutuma ambazo zilielekezwa kwake kuhusu utengaji wa mgao mkubwa wa bajeti katika eneobunge lake la Kiharu  Ndindi alikanusha akisema kuwa hio ilikuwa ni masuala ya siasa tu hayana msingi wowote.

Ndindi Nyoro aliweza kusema kuwa siku ya  mwisho aliweza kuzungumza na kiongozi wa taifa Oktoba 2024 mwaka jana, hata hivyo alisema kuwa utekelezaji wa masuala ya bajeti ni jambo ambalo huchukua muda bali si jambo linalokamilishwa tu kwa haraka.