Jiji la Nairobi linatarajiwa kuwa na msongamano wa magari Juma hili hii ni kutokana na ujio wa mfalme kutoka taifa la Uholanzi na Lesotho bwana Willem-Alexanderr na mfalme Letsie wa Lesotho.

Mnamo Jumatatu ya Machi, 17, 2025 usiku mfalme na malkia wa Taifa la Uholanzi Willem -Alexanderr na Malkia Maximawill walizuru Kenya kama wageni wa Rais Ruto katika ikulu ya Nairobi.

Siku ya Jumanne Machi 18,2025 Mfalme na Malkia kutoka Uholanzi wataweza kuzuru  na  kuwa  na safari nyingi katika jiji la Nairobi watafanya shughuli mbalimbali ikiwemo Upanzi wa miti,ambapo huenda ikafanya  na kusababisha msongamano wa magari jjini.

Siku hiyo ya Jumanne ya Machi 18,2025   mfalme wa Lesotho  bwana Letsie  atawasi Nchini kwa mwaliko rasmi na kwa shughuli maalumu za kikazi.

Kwanzia Machi 17,2025 hadi 21 Machi,2025 barabara ya city itasalia kufungwa ili kuruhusu majaribio ya mbio za safari rali  ambazo zinatarajiwa kuanza kufanyiwa majaribio karibu  na afisi ya Gavana jijini Nairobi.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Siku ya Jumatano msafara huo utaelekea eneo la Naivasha  kupitia Barabara ya Maimahiu na kurudi, msafara ambao utafanya malori ya kubeba mizigo yatumie njia mbadala kwa ajili ya usafiri ambao kwa namna moja au nyingine utakuwa umekabiliwa na msongamano wa magari mengi yatakayokuwa yakielekea Naivasha.

Mfalme wa Lesotho Jumatano Machi 19,2025 atazuru kampuni ya Udongo katika mji wa Ruiru  na shule ya Ruiru kwa shughuli ya Upanzi wa  miti kabla ya kupanga kuondoka siku itakayofuata.

Vilevile Safari hiyo pia itashuhudia msafara mrefu Pamoja na mlolongo wa magari katika Barabara Kuu ya Thika kwa ajili ya kupisha shughuli hio adhimu na ya kihistoria nchini.

Viongozi hao wataondoka nchini mnamo Alhamisi  Machi 20, 2025 kutumia Barabara kuu za Uhuru na Barabara ya Mombasa ambapo pia katika pilikapilika zao za kuondoka nchini kutatarajiwa kushuhudiwa misongamano ya magari kwa ajili ya kuwapa nafasi murwa ya kuondoka wakielekea katika uwanja wa kimataifa wa  ndege wa Jomo Kenyatta.

Wageni hao wanapoondoka siku ya Ijumaa kutakuwa na Kilele cha  Mashindano ya safari Rali mtaa wa Naivasha ambapo kwa ukurasa huo huo pia huenda msongamano wa magari ukashuhudiwa kwa viwango vikubwa, hio itaashiria juma hili litakuwa lenye shughuli nyingi nchini Pamoja na misongamano ya magari.