caption
Mfalme wa Uholanzi Willem Alexander ambaye aliwasili nchini Kenya Jumatatu 17, Machi ameahidi kukutana na vijana wa nchi ya Kenya kabla ya kukamilisha ziara yake ya siku tatu katika taifa hili.

Kiongozi huyo wa serikali ya uholanzi amesema kwamba yeye pamoja na rais wa taifa la Kenya William Ruto watakutana na vijana na kuwasikiliza na haki yao pia lazima iheshimiwe.

"Asubuhi hii kwenye ubalozi tutakuwa tunakutana na vijana wa Kenya ili kusikiliza maoni yao kuhusu maendeleo.  ili tupate nafasi ya kuona kuelewa na kujenga maisha yao ya baadaye katika taifa ambalo wanalipenda. Maisha ya baadaye ambayo kila mtu anafaa kuhusishwa kwa usawa," alisema Mfalme huyo.

Tunamini katika maisha ya baadaye ya wakenya, baadaye ambayo itakuwa furaha kwa wakenya wote ambao asilimia yao ni ya miaka 20. Taifa linaamini kwa mawazo yao kuhusu vijana wa taifa zaidi ya milioni moja. Watu wa Kenya kama tu wale wa Uholanzi wanataka haki yao kama wananchi na inafaa kuheshimiwa na sauti yao isikilizwe," aliendela rais huyo.

Wakati huo amefurahishwa na ziara yake nchini akiitaja kama mwanzo wa mahusiano mema baina ya nchi hizo mbili na wanaangalia zaidi kusaidiana tena na tena katika shughuili mbalimbali. ameeleza kwamba yatasaidi kuku maendeleo kati ya Kenya na Uholanzi.

"Nimefurahishwa kwamba mataifa yote mawili yamekuza uhusiano hasa zaidi katika ziara hii. Mahusiano kama ya haki za kibinadamu, uongozi na uwajibikaji. Tumefurahia kupata nafassi hii ili kujadili na kuafikiana  kuhusu sehemu hizi," alisema 

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

"Kuzuru hapa kunaashiria makubaliano na kuzungumza kati yetu. Tuko maakini sana kuangazia siku zijazo ambazo zitakuwa na nafasi nzuri bwana rais kukutana na wakenya kutoka tabaka mbalimbali miongoni mwa mataifa haya yote mawili,' alieleza. 

Willem-Alexander Claus George Ferdinand [Alizaliwa 27 Aprili 1967) amekuwa mfalme wa Uholanzi tangu 30 Aprili 2013.

Willem-Alexander anazungumza Kiingereza, Kihispania, Kifaransa, na Kijerumani (lugha ya asili ya baba yake) pamoja na Uholanzi yake ya asili. Anawakilisha ufalme nyumbani na nje ya nchi.

Katiba inampa mamlaka  mfalme kuteua, kuwafuta kazi na kuwaapisha mawaziri wote wa serikali na makatibu wa serikali.Kama mfalme, yeye pia ni Rais wa baraza la nchi.